fungua hapa kupata video,☝️Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika Halmashauri ya Meru.
Zoezi la malipo katika Halmashauri ya Meru limefanyika leo katika Kata ya Usa-River, Ambureni, Imbaseni, Maji ya Chai, Poli, Singing, Nkonrua, Nkoaranga na Songoro.
Walengwa hao wa mpango wa kunusuru Kaya Masikini TASAF 7,752 wamelipwa fedha shilingi 301,444,000.00 mbapo kati ya fedha hizo shilingi 248,076,000.00 zimelipwa taslimu na shilingi 53,368,000.00 zimelipwa kwa njia ya mtandao.
Kwa niaba ya walengwa wa mpango huo, Bi. Vicky J. Massawe ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya Sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa msaada huo kwani fedha wanazozipata zinawasaidia kusomesha watoto na kufanya miradi midogomidogo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa