Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, amesema Serikali imefuta Shamba la Valeska lenye ekari 4087 kwa manufaa ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Aidha, Mhe.Lukuvi ameeleza kuwa Serikali imeelekeza kuwa jumla ya ekari 1500 zitagawia kwa Vijiji 3 vya Kwaugoro, Maroroni na Valeska vinavyopakana na Shamba kwa mgawanyo wa ekari 500 kila Kijiji. Pia Serikali imeelekeza ekari 1028 zitatumika kwaajili ya kilimo na ekari 1659 zitatumika kwaajili ya makazi na biashara.
Mhe. Lukuvi amewataka Madiwani wa Halmashauri hiyo kusimamia mgawanyo wa Shamba hilo kwa maslahi mapana ya Halmashauri.
Aidha, katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mhe.Lukuvi ametoa tamko la kufuta waraka namba moja wa Ardhi uliotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwa unawanyima haki Madiwani kushiriki katika upangaji wa Ardhi kwenye maeneo yao. "wataalam wawashauri Madiwani ili wafanye maamuzi sahihi na si kuwapangia " amehimiza Mhe Lukuvi
Aidha, Mhe.Lukuvi amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuwatumia Wataalamu wa Ardhi na kuwawezesha Kutekeleza majukumu yao.
Mhe.Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ameishukuru Serikali na kuahidi kutekeleza maagizo ya Mhe .Waziri ambapo utekelezaji umeanza kwa kuwa na kikao na Madiwani mara baada ya ziara ya Mhe. Waziri Lukuvi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mhe.Jeremia Kishili ametoa wito kwa Madiwani kushirikiana kupanga Shamba hilo sambamba na kuwaelimisha Wananchi kwani ugawaji wa Shamba hilo unalenga kupunguza changamoto za uhaba wa Ardhi na kuongeza mapato ya Halmashauri kwa maendeleo ya Wananchi.
Akishukuru kwa biaba ya Waheshimiwa Madiwani Mhe.Shari Pallangyo ameishukuru Serikali kwa kufuta Shamba hilo na kueleza kuwa wapo tayari kufanyia kazi Maelekezo yaliyotolewa na Serikali.
Ikumbukwe kuwa kabla Serikali kutoa Maamuzi hayo, Shamba hilo lilikuwa linamilikiwa na Chama cha Ushirika(ACU).
Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Jeremia Kishili, Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg.Emmanuel Mkongo na wakwanza kulia ni Karibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Mchembe
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa Mkutano wa Waziri Lukuvi na Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati Mkutano
Wataalam Ngazi ya Mkoa,Wilaya na Wananchi wakati wa Mkutano
Watumishi wa Halmashauri wakati wa Mkutano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa