MERU Kazi iendelee...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mhe.Rais.Samia Suluhu Hassan imetoa Shilingi Bilioni 2.16 kwaajili ya ukamilishaji wa miundombinu katika Sekta ya Elimu Sekondari na Msingi pamoja na Sekta ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa Mchanganuo ufuatao:
Bilioni 1.45 Sekta ya Elimu Sekondari*
Serikali imetoka Shilingi Bilioni 1.4 kwaajili ya ujenzi na ukamilishaji wa vyumba 70 vya Madarasa katika Shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru.Pia hivi karibuni ilitoa shilingi Milioni 50 kwaajili ya ukamilishaji wa maboma manne katika Shule mbili za Sekondari Muungano na Umoja King'ori.
Milioni 550 sekta ya Afya
Hamashauri ya Wilaya ya Meru ni miongoni kwa Halmashauri 75 nchini zilizotengewa Shilingi Milioni 300 kwaajili ya Ujenzi wa majengo ya huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya iliyopo Pembezoni mwa barabara ya Arusha -Holili ambavyo inakabiliwa na ajali nyingi za barabarani,
Pia.Serikali imetoa Shilingi Milioni 250 kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Mareu.
Milioni 160 Sekta ya Elimu Msingi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru imetengewa Shilingi Milioni 160 za ujenzi Wa mabweni 2 katika Shule za Msingi zenye Wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa