Naibu waziri wizara ya afya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt.Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha afya Momela kilichopo Halmashauri ya Meru ,Wilayani Arumeru kufuatia mgogoro uliopelekea kuondolewa kwa baadhi ya huduma kutokana na Wafadhili wa kituo hicho Shirika la Africa Amini Alama kuondoa baadhi ya mashine ,ameliagiza shirika hilo kurejesha mashine zote zilizokuwa zikitumika katika kituo hicho ndani ya siku 7 ili wananchi waendelee kupata huduma zote zilizokuwa zinatolewa hapo awali.
Naibu waziri ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara ya wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki ,ikiwa ni baada ya kikao kati ya uongozi wa Wilaya ya Arumeru,Uongozi wa Halmashauri na wafadhili wa Shirika la Africa Amini Alama ambapo alieleza kuwa serikali yaTanzania ipo tayari kufanya ushirikiano na wadau wa afya kwa kuzingatia Sheria,kanuni ,taratibu na miongozo ya sekta hiyo.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kilipo kituo hicho Dkt. Maneno Focus, Kituo cha afya Momela kimesajiliwa ni mali ya umma na kina watumishi wa Serikali na hupokea dawa toka Bohari ya dawa pamoja na fedha za wahisani mbalimbali zikiwemo fedha za Busket fund.
Aidha, taarifa imeonesha mwaka 2009 kijiji cha Olkung'wado kilitenga ekari 10 za ardhi kwaajili ya ujenzi wa zahanati iliyokamilika 2010 na kukabidhiwa Serikalini ambapo ilisajiliwa mwaka 2012 kama zahanati ya kijiji cha Okungwado momela na mwaka 2013 Serikali iliingia makubaliano ya uboreshaji Zahanati hiyo na wafadhili wa Africa Amini Alama. Mnamo mwaka 2015 Zahanati hiyo ilipandishwa hadhi kuwa kituo cha afya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg.Emmanuel Mkongo katika kikao alisema Halmashauri hiyo ilishindwa kuridhia ombi la wafadhilli la kubadilisha Kituo cha afya Momela ambacho ni cha Umma (public) kuwa Hospitali ya binafsi ya wahisani (Charitable private Hospital) kwakuwa ni kinyume cha Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo za uendeshaji na usimamizi wa Vituo vya kutolea huduma.
Mkongo alisema Halmashauri inathamini mchango wa wafadhili wa Africa Amini Alama na ilitaka kumaliza changamoto zilizojitokeza kwa kushirikisha Mamlaka mbalimbali za Serikali kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo za uendeshaji na usimamizi wa Vituo vya kutolea huduma.
Mhe.Ndugulile baada ya kikao ametoa mwelekeo wa Serikali kuwa, kituo hicho kitabaki kuwa mali ya umma na kitakapokidhi vigezo kitapandishwa hadhi kuwa Hospitali ya umma na siyo ya binafsi kama wafadhili walivyoomba, ”hatuwezi kutoa kituo cha umma kwa mtu binafsi”amesisitiza Ndugulile.
Kwa upande wa Wafadhili Christine Wallner ambaye ni Rais wa Shirika la Afrika Amini Alama ameishukuru serikali kwa kutatua mgogoro huo na kueleza kuwa shirika lipo tayari kuendelea kufadhili kituo hicho sambamba na kutekeleza agizo la kurejesha mashine maeneo husika. Pia ameiomba Serikali kuharakisha maandalizi ya makubaliano ya kuboresha utoaji huduma Kituoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amemuomba Mhe. Naibu waziri kupokea ombi la Wananchi la kukipandisha hadhi kituo hicho cha afya kuwa Hospitali ili kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za afya, pia ametoa wito kwa wananchi kutokuwa sehemu ya kuchochea migogoro .
Mhe. Mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki, Dkt.John D. Pallangyo ameishukuru Serikali namna inavyowathamini wananchi wake kwa kufanyia kazi ombi lao alilowasilisha la kuomba utatuzi huduma kusitishwa katika kituo hicho cha afya.
Nao Wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki wameiomba Serikali kuharakisha mpango wa kuandaa makubaliano ya uendeshaji wa kituo hicho pamoja na kukipandisha hadhi kuwa Hospitali.
Naibu waziri wizara ya afya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt.Faustine Ndugulile akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ya wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki.
Naibu waziri wizara ya afya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt.Faustine Ndugulile akizungumza kwenye kikao cha Uongozi wa Wilaya ya Arumeru,uongozi wa Halmashauri ya Meru na Wafadhili.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru , Jerry Muro akizungumza wakati wa mkutano wa Mhe.Naibu waziri na wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki.
Wakwanza kushoto mwa Mhe .Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile ni, Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Wedson Sichalwe na pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg.Emmanuel J. Mkongo.
Mhe. Mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki, Dkt.John D. Pallangyo akizungumza wakati wa Mkutano na wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki.
wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki wakati wa Mkutano.
Christine Wallner ambaye ni Rais wa Shirika la Afrika amini alama akizungumza wakati wa mkutano wa Mhe.Naibu waziri na wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki.
wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki wakati wa Mkutano
Cornelia Wallner ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Afrika amini alama akizungumza wakati wa mkutano wa Mhe.Naibu waziri na wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki.
wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki wakati wa Mkutano.
wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado Kata ya Ngarenanyuki wakifurahia maamuzi ya Serikali.
Ndg. Mollel akizungumza wakati wa Mkutano
Naibu waziri na viongozi alioambatana nao akitembela kitou cha Afya Momela
Dkt. Veronica Gisambo akitoa maelezo kwa Naibu waziri wizara ya afya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt.Faustine Ndugulile akitembela kituo cha Afya Momela .
aliyeshika Karatasi Nyeupe ni,Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Maneno Focus,
Naibu waziri akimsalimu mmoja wa wagonjwa alipotembelea kituo cha Afya Momela .
Naibu waziri na viongozi alioambatana nao akitembela kitou cha Afya Momela
Naibu waziri Dkt.Faustine Ndugulile akikagua vifaa akitembela kitou cha Afya Momela
Naibu waziri Dkt.Faustine Ndugulile akitembela kituo cha Afya Momela .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa