Akizungumza wakati wa uzinduzi wa taarifa ya utafiti ya uliofanywa na shirika lililopo chini ya Twaweza la Uwezo Tanzania kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru mwaka 2015 juu ya mradi ulio anzishwa na Serikali ili kumwezesha mwanafunzi kujua kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK ) kabla ya kufika darasa la 3 ,Kaimu mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Idd Kimanta amezikumbusha Serikali za vijiji kutekeleza jukumu la kuhakikisha maendeleo ya shule ni ajenda ya kudumu kwenye vikao kwani huwezi kujadili maendeleo ya shule bila kujadili uwezo wa wanafunzi kujua kusoma,kuandika na kuhesabu yaani (KKK) pia amesema mbali na changamoto zilizopo ,serikali imetengeneza mazingira rafiki ya elimu bora kwa kutatua changamoto ya wanafunzi kukaa chini pamoja na kutoa fedha za ruzuku (capitation fund) kwenye shule za msingi na sekondari pia na kuwezesha madarasa ya awali kuzungumza.
Diwani wa Kata ya Nkoaranga Zephania Mwanuo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya elimu,afya na maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru amepongeza uanzishwaji wa mradi wa KKK pia ametoa rai kwa wazazi kutimiza wajibu wao kwenye elimu kwani wengi wamekua wakikimbizana na harakati za maisha bila kufuatilia mwenendo wa kielimu wa watoto wao.
Naye mthibiti mkuu wa ubora wa shule kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Onesmo J. Oleteipa amesema idara ya elimu itatumia taarifa hiyo ya utafiti kama nyenzo na kuweka mikakati ya utatuzi wa mapungufu yaliyo jitokeza kufafanua kuwa kunatofauti kubwa kwenye uhalisia wasasa kwenye matumizi ya KKK na taarifa ya utafiti uliofanywa na twaweza kwani ni wakipindi kirefu miaka 3 akithibitisha hilo ametoa mfano " Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Christopher J. Kazeri alitoa agizo kwa watendaji wa vijiji Kudhibiti mahudhurio ya wanafunzi jambo lililozaa matunda ambapo kwa utafiti wa idara ya elimu uliofanyika mwaka huu 2018 umeonyesha mahudhurio ya wanafunzi kuwa zaidi ya asilimia 85.
walimu waliohudhuria uzinduzi huo wameshauri ni muhimu walimu kujengewa uwezo wa kutosha kufundisha madarasa ya awali ambayo ndio msingi mkuu wa KKK.Mmoja wa walimu hao Mwl. Asina R. Mkilindi ameomba Serikali somo la kingereza linaloanza kufundishwa kuanzia darasa la 3 kuanza kufundishwa kuanzia darasa la kwanza kwani kwa sasa walimu ni wengi wanaotolewa kwenye shule za sekondari kufundisha msingi.
Naye mzazi Samweli Imani amesema yeye kama mzazi atashirikiana na walimu ili kuhakikisha mtoto wake anajua kusoma na kuandika na kuhesabu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa