Halmashauri ya Wilaya Meru kupitia fedha za mapato yake ya ndani (Own Source) imetumia zaidi ya Shilingi Milioni 160 kununua vifaa vya ujenzi. Vifaa hivyo vinajumuisha Bati 1860 yaliyonunuliwa kwa shilingi 48,259,004.51,Mbao shilingi 64,598,752.00 na Saruji mifuko 3325 kwa shilingi 48,212,500 kwaajili ya ukamilishaji wa vyumba vya Madarasa.
Mikakati hii ya ununuzi wa vifaa kwa jumla (bulk procurement) ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021 wanaanza masomo mapema.
Aidha, katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru idadi ya wanafunzi 6,851 walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kati yao 5216 wamepangwa kwa awamu ya kwanza na 1,635 wanasubiri kupangwa kwa awamu ya pili baada ya vyumba vya madarasa kukamilika.
Aidha , kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza kutokana na kupanda kwa ufaulu kutoka asilimia 92.02 mwaka 2019 hadi 93.22 katika mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka 2020. Bofya
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa