Halmashauri ya Wilaya ya Meru imepokea ugeni kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali WILDAF ( Women in Law and Development in Africa) lenye makao yake makuu Dar-es-salaam. Shirika la WILDAF Lina Lengo kuu la kumuinua Mwanamke katika Nyanja zote katika Jamii, kiuchumi, Kisiasa,Kifikra,Kiutamaduni n.k
Aidha Shirika la WILDAF Lina Lengo la kutekeleza mradi wa kujenga ushirika wa Wanawake katika Maswala ya Uongozi (SIASA NA URAIA) Kwa kutumia Makundi mbalimbali kama Viongozi wa Dini na Makundi maalumu.
Hii yote Lengo kuu nikutaka kuongeza wigo mkubwa wa ushiriki wa Wanawake katika Maswala ya Uongozi hasa katika chaguzi zilizoko mbele yetu.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Frola Msilu ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Meru ameahidi kutoa ushirikiano wa hali na Mali ili kuweza kuongeza ushawishi wa ushiriki wa Wanawake katika Chaguzi zilizoko mbele yetu na hata kuwafanya wanawake kuwa mstari wa mbele katika Maswala ya Uongozi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa