Shule ya Sekondari Kisimiri ambayo ni shule ya Serikali ya Kata iliyopo Halmashauri ya Meru ,Wilayani Arumeru Mkoani Arusha ndio shule ya Sekondari bora kati ya shule 594 Nchini Tanzania.
Ubora wa Kisimiri umetokana matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2019, jumla ya wanafunzi 60 waliofanya Mtihani huo kati yao 58 wamepata ufaulu wa daraja la kwanza na wanafunzi wawili tu ndio waliopata daraja la pili.
Mbali na ufaulu wa madaraja kwa wanafunzi, shule hiyo imeongoza kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza katika masomo 3 ambayo ni Kingereza, Histori na Kemia. Pia katika somo la Fizikia na Hisabati imeshika nafasi ya tatu kitaifa.
Jumla ya wanafunzi 4 wa shule hiyo wameweza kuingia kwenye kumi bora kitaifa wakiongozwa na Mwanafunzi wa kwanza kitaifa kwenye masomo ya Sayansi Hermani Mugisha sambamba na kutoa wanafunzi bora 2 wautafiti wa kisayansi.
Mkuu wa Shule hiyo Mwl.Valentine Tarimo amesema Serikali imechangia kwa kiasi kikubwa shule hiyo kufanya vizuri kwa kugharamia kwa asilimia 100 chakula cha wanafunzi hao wa kidato cha tano na sita ambapo zaidi ya milion 72 hutumika kila mwaka pamoja na kuboresha miundombinu kupitia mradi wa P4R shule ilipewa zaidi ya milioni 500 za ujenzi wa mabweni 2,madarasa 8 vyoo vya matundu 10 na miradi hii yote imekamilika.
Mwl Tarimo amesema uongozi wa shule hiyo umejiwekea mkakati uitwao (Ufaulu mzuri) unaolenga walimu kufundisha kwa malengo na kusimamia malengo yao kwa wanafunzi hao kupata matokeo mazuri ambao umekua na mafanikio makubwakwani kwa kipindi cha miaka 3 mfululuzo ufaulu wa kidato cha sita umekua ukiongezeka, ambapo mwaka 2017 shule hiyo ilishika nafasi ya 3 kitaifa, 2018 ikawa ya 2 na mwaka huu imekua ya kwanza.
Mwl Tarimo amesema ufundishaji mzuri wa walimu, utayari wa wanafunzi,usimamizi mzuri wa bodi ya Shule,Ushirikiano kutoka Halmashauri ,Mahusiano Mazuri ya Jamii inayozunguka shule, mchango wa wadau wa Elimu (friends of Kisimiri) vimepelekea kupata matokeo hayo.
Aidha Tarimo mbali na shukuru Serikali kwa kuajiri walimu 3 wa masomo ya sayansi ameomba kuongezewa Walimu wa masomo hayo kwa kuwa bado kuna uhitaji.
Shule hiyo ya Kisimiri yenye walimu 55 wanafunzi 1000 na watumishi wasio walimu iliyopo umbali wa Km 37 toka makao makuu ya Halmashauri ya Meru , kwa sasa nui gumzo Nchini Tanzania.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa