Wanafunzi 136 wenye Mahitaji Maalumu kunufaika na elimu ya Sekondari baada ya kuanza rasmi kwa shule ya Sekondari ya mfano nchini ya Patandi Maalumu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru, Mkoani Arusha.
Ndugu Emmanuel Mkongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru , ameishukuru Serikali kwa kwa kujenga miundombinu ya madarasa ,mabweni,ofisi ya walimu ,maabara, na
maktaba kwani ni sehemu ya mafanikio makubwa katika kuhakikisha kila mtoto wa Tanzania anapata elimu wakiwemo watoto wenye Mahitaji Maalum yanatimia.
Mkongo amepongeza juhudi za timu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI , Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia pamoja Wataalam wa Chuo Cha Ualimu Patandi na Wataalam wa Halmashauri katika kuhakikisha miundo mbinu muhimu na rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum inakamilika.
Mkongo ametoa wito kwa Wazazi wa wanafunzi waliopangwa shule hiyo kuhakikisha wanaripoti kwa wakati na ili wanafunzi waweze kuanza masomo.
Shule ya Sekondari Patandi Maalumu imepangiwa wanafunzi 185 wakiwemo wanafunzi wa Kutwa 49 na wanafunzi wa bweni wenye mahitaji maalum 136.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa