• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

SIKU YA WANAWAKE YAADHIMISHWA KWENYE HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU

Imewekwa: March 24th, 2018

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila tarehe 8 machi  ya kila mwaka yame adhimishwa leo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kutoa mafunzo kwa wanawke 150 ambao ni viongozi wa vikundi  77 vilivyo nufaika kupewa fedha kiasi cha sh.181,500,000 za mikopo na Halmashauri hiyo kutoka kwenye mfuko wa mikopo ya wanawake na vijana kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo mwakilishi wa Katibu tawala Wilaya ya Arumeru ambaye ndiye mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Magdalena O. John ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha sheria kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema wanawake ni chachu ya maendeleo hivyo ni muhimu kutumia fusra za mikopo wanayopewa kujikwamua kiuchumi  kwa kufanya shughuli za kiuchumi  zitakazo inuwa vipato vyao na kushiriki uchumi wa viwanda.

Aidha mwanasheria Magdalena amesema Serikali  katiaka kutekeleza kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani ambayo ni "Kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini" Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo( NMB) imeandaa mafunzo mbalimbali kama vile ujasiriamali yatakayotolewa kwa wanawake hao kwa lengo la kuwajengea uwezo wa matumizi sahihi ya  mikopo wanayopewa kujikwamu kiuchumi hivyo amewasihi kutumia mafunzo hayo na kuwafundisha wanawake wengine ambao hawajaudhuria mafunzo hayo.


Mwakilishi wa Katibu tawala Wilaya ya Arumeru ambaye ndie mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Magdalena O. John ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha sheria akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

baadhi ya wanawake ambao ni viongozi wa vikundi  vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru  toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru   .


baadhi ya wanawake ambao ni viongozi wa vikundi  vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru  toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru   .


baadhi ya wanawake ambao ni viongozi wa vikundi  vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru  toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru   .


baadhi ya wanawake ambao ni viongozi wa vikundi  vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru  toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru   .

Wanawake ambao ni viongozi wa vikundi  vilivyonufaika kupewa mkopo na Halmashauri ya Wilaya ya Meru  toka kwenye mfuko wa wanawake na vijana wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru   .

Mtoa mada ya ujasiriamali ,Saumu s. Kweka ambaye ni Mratibu wa dawati la uwezeshaji wanachi kiuchumi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza na wanawake kuwa ili wawe wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu na kujenga mausiano mazuri na wafanyabiashara wengine .

Hermelinda Kasihwaki ambaye ni Meneja wa Benki ya NMB tawi laUsa-River ameto elimu kwa wanawake juu ya faida ya kutumia benki kuifadhi fedha kuwa ni njia salama na inaepusha matumizi mabaya ya fedha.

Afisa lishe kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru Asia Ijumaa katika utoaji wa mada inayohusu mtindo bora wa maisha amewashauri wanawake kujali afya zao kwa kutumia mlo wenye makundi yote matano ya chakula ambayo yatawapa virutubisho vinavyoitajika mwelini na kuepuka magonjwa yatokanayo na ulaji.

"umuhimu wa kupima ukimwi utakuwezesha kujua afya yako ikiwa hujaathirika utajilinda na kama umeathirika utapewa njia sahihi zitakazo kuwezesha kuishi zaidi na kuepuka maambukuzi mapya "amesema Mratibu wa UKIMWI  kwenye Halmashauri ya Meru Grace Mghase wakati wa maadhimisho wa siku ya wanawake kwenye Halmashauri hiyo pia amewasihi wanawake kutokaa kimya bali kuwaelimisha vijana na familia kwa ujumla kujinga na UKIMWI .

mbali na kuwa mwakilishi wa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye Halmashauri ya Meru mwanasheria (wakili) Magdalena O. Johnametoa mada ya wanawake na umilikiwa wa ardhi,sheria ya ndoa na miradhi.

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa