Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro ameiomba Serikali kuwezesha ujenzi wa stendi ya kisasa ya Mabasi Maadira iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani humo kwa kueleza kuwa mradi huo unamanufaa makubwa kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo pindi utakapoanza utatoa ajira kwa vijana na ukikamilika utaongeza hali ya kipato , kuboresha hali za maisha na kuongeza mapato yatakayotumika kuboresha huduma mbalimbali katika sekta ya Afya ,Elimu na Maji.
Aidha Muro ametoa ombi kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Eng.Joseph Nyamhanga wakati wa ziara yake Wilayani humo kwa kumsihi kupitisha andiko la mradi huo wa ujenzi Stendi ya Mabasi Madiira katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, nakueleza kuwa ni wenye manufaa makubwa kiuchumi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Akisoma taarifa ya Mradi wa Stendi ya Mabasi Maadira, Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bw. Maarufu Mkwaya ameeleza kuwa Halmashauri hiyo iliwasilisha andiko la kuomba bilioni 10 Kama awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi huo ambao ukikamilika utatoa huduma kwa wananchi ikiwemo ya mabasi ya mikoani, kituo cha daladala, kituo cha taxi pamoja na maduka na huduma za kibenki pia mapato ya zaidi ya Shilingi bilioni 2.6 yatapatikana kila mwaka.
Eng.Joseph Nyamhanga amesema Serikali inania thabiti ya kuwaletea maendeleo wananchi wake kwani kwa awamu ya pili imetoa Shilingi Bilioni 137.3 kwaajili ya ujenzi wa Miradi ya kimkakati kwenye Halmashauri mbalimbali Nchini.
Naye MKurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo amesema mradi huo utaleta tija kwenye utoaji wa huduma kwenye halmashauri hiyo ambapo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ilikusanya mapato ya Shilingi bilioni 3.2 sawa na asilimia 81 ya lengo la mwaka hivyo mradi huo wa stendi ya madiira utaiwezesha Halmashauri kukusanya mapato ya kutosha na kutoa huduma bora kwa wananchi wake.
ziara ya Katibu Mkuu ofisi ya Rais TAMISEM Eng.Joseph Nyamhanga eneo la madira .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akielezea ujenzi wa Stendi ya Madira kwa Katibu Mkuu ofisi ya Rais TAMISEM Eng.Joseph Nyamhanga(wa pili kushoto)
Afisa Mipango Halmashauri ya Meru Maarufu Mkwaya
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa