Kanisa la Pentecoste Ngulelo launga Mkono uboreshaji wa Sekta ya Afya Wilayani Arumeru kwa kuchangia vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi milioni 9.
Kiongozi wa Kanisa hilo Mwalimu Onesmo Nnko amesema hatua hiyo ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg. Jerry Muro vifaa vilivyonunuliwa kutokana na sadaka za waumini na viongozi ni katika kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya kanisa na Serikali.
Mwl. Onesmo Nnko amesema wao kama kanisa hawana budi kuungana na serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya ili kutengeneza jamii bora .
Aidha vifaa vilivyotolewa na Kanisa hilo ni Vitanda 6 vya wodini, Vitanda 2 vya uchunguzi, Machela moja, Mtungi mmoja wa Hewa ya Oksijeni , Mashuka 100, Seti 3 za kujifungulia , Mashine 3 za kupima shinikizo la damu, mashine moja ya kusafishia njia ya hewa, Magodoro madogo 8 kwa ajili ya chumba cha watoto waliozaliwa chini ya miezi 9 ( njiti ) na Mapazia 2 ya Hospitali .
Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndg. Jerry Muro amesema ,kupatikana kwa vifaa hivyo kutasaidia kuimarisha huduma pamoja na kuondoa changamoto ya uhaba wa vifaa vya kutolea huduma.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Meru, Dkt. Maneno focus amesema kwa sasa huduma za afya zinazidi kuimarika na wameamua misaada hiyo itolewa katika kituo cha afya cha usa river ambacho Mhe Rais Magufuli alitoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya 6 na kukarabati majengo 3, ujenzi ambao ulishakamilika na kituo kinatoa huduma za kisasa .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa