TAHAPAO ( TASWIRA YA HAKI PARALEGAL ORGANISATION) Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Meru wametoa Elimu Kwa viongozi wa kamati za Mtakuwa Kata ya Usa-River na Imbaseni na kuahidi kusaidia kamati hizi katika kupambana na Ukatili wa kijinsia Kwa Wanawake na Watoto. Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Mtoto na Jinsia Martha Mzava Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl Zainabu Makwinya ameipongeza Taasisi ya TAHAPAO Kwa Mafunzo waliyoyatoa na kuwataka wasimamizi ngazi za Kata kwenda kusimamia wasaidizi wao wa Ndani ya Kata na kuhakikisha wanatoa ushirikiano Kwa Taasisi hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yakusaidia Wananchi. Aidha Mkurugenzi wa Taasisi ya TAHAPAO Sifaeli R. Pallangyo ameomba ushirikiano hasa katika Taasisi za Serikali ikiwemo Hospitali, Vituo vya Polisi ili wanapokumbana na matatizo yanayohitaji uharaka wa Taasisi hizo iwe rahisi kutatuliwa. Vile vile Afisa Ustawi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Restusta Mvungi amewataka Viongozi wanaosimamia Maeneo mbalimbali kutoa Taarifa za haraka pindi zinapo tokea ili kutoa msaada wa haraka na kuchukua Hatua za haraka pindi matatizo hayo yanapo jitikeza.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa