Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya ya Arumeru, imezitaka Halmashauri za Wilaya hiyo ( Arusha na Meru ) kuhakikisha zinaimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato ikiwa ni pamoja na kuzuia mianya ya upotevu wa mapato hayo na ubadhirifu fedha za umma.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru, Bw. Deo Mtui, ametoa rai hiyo wakati wa kikao na wahusika wa Ukusanyaji mapato kutoka Halmashauri za Arusha na Meru kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Patandi maalumu ambapo amesema uchambuzi wa mfumo wa kukusanya mapato kwa kutumia mashine za kielekroniki (POS) uliofanywa na Taasisi hiyo umebaini mapungufu kadhaa "Ipo haja ya kuongeza juhudi na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali, kwani tunaona kuna mapungufu katika eneo hili " Amesema Bw. Mtui.
Vilevile Mtui ameeleza mapungufu yaliyojitikeza katika uchambuzi uliofanywa na Taasisi yake ni pamoja na baadhi ya wakusanya mapato kuchelewa kuwasilisha fedha benki hivyo kuathiri ukusanyaji wa mapato.
Mtui amehimiza ni muhimu kwa Halmashauri ,Mawakala na wote wanaohusika kukusanya mapato ya Serikali kuzingatia Sheria Kanuni na taratibu za fedha za umma kwani kutozingatia hayo kunapelekea kuvunja sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2017 .
Mtui, amesema Wakusanya mapato wa Halmashauri za Arusha na Meru ambao ni Mawakala na Watumishi wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za ukusanyaji mapato ambazo zinawataka kuweka fedha Benki kila siku, kwani kutokufanya hivo ni uvunjaji wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rusha ya Mwaka 2017, kifungu cha 28 ambacho ni kosa la Ufujaji na Ubadhirifu sambamba na kifungu cha 31 ambacho ni matumizi mabaya ya madaraka.
Kikao hicho cha Warsha ya siku moja ambacho kimewajumuisha Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili , waweka Hazina, Maafisa TEHAMA, Wakakuzi wa Ndani, Maafisa Mapato, Mawakala na wakusanyaji mapato zaidi ya 176, kimeweka maazimio ya kuhakikisha fedha za makusanyo yote ya Halmashauri zote mbili zilizocheleweshwa kuwekwa benki kuwekwa benki kabla ya tarehe 05 Oktoba 2022.
Vilevile kikao hicho kimeazimia mikakati mbalimbali itakayochochea ukusanyaji mapato na kuwaletea wananchi maendeleo .
Arumeru Kazi iendelee.....
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru, Bw. Deo Mtui akizungumza wakati wa kikao
Wahusika wa Ukusanyaji mapato kutoka Halmashauri za Arusha na Meru
wahusika wa Ukusanyaji mapato kutoka Halmashauri za Arusha na Meru
wahusika wa Ukusanyaji mapato kutoka Halmashauri za Arusha na Meru
Maafisa wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru
wahusika wa Ukusanyaji mapato kutoka Halmashauri za Arusha na Meru
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa