Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru Bw. Deo Mtui ametambulisha Proramu ya TAKUKURU -Rafiki Kwa Viongozi wa watoa huduma ya usafirishaji wa Bodaboda katika Wilaya ya Arumeru.
Katika kikao cha watoa Huduma ya usafiri wa bodaboda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru alipata nafasi ya kutambulisha Programu ya TAKUKURU- RAFIKI ambayo ni mkakati wa Taifa ili kupanua wigo wa mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwa Kuongeza Ushiriki wa Wananchi na Wadau katika kupambana na vitendo vya Rushwa.
" Nichukue fursa hii kuwajulisha kuwa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeanzisha program ya TAKUKURU RAFIKI ambayo inatoa fursa kwa wananchi na kuwa *Huru* zaidi kutoa taarifa za Mianya ya Rushwa tofauti na hapo zamani TAKUKURU ilikuwa mbali na Wananchi hivyo kushindwa kutoa Ushirikiano." Amesema Mkuu wa TAKUKURU.
Aidha, amesisitiza kwa viongozi wa watoa huduma ya usafirishaji wa bodaboda kurasimisha vijiwe vyote na kuwatambua wasafirishaji wa bodaboda ili kuweza kukaa nao kwa pamoja na kuweza kutambulisha programu hii ya TAKUKURU RAFIKI ili kuweza kutatua kero wanazokutana nazo na kuzuia mianya yote ya Rushwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa