Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Ndg.Deo Mtui ambaye ni Mkuu wa TAKUKURU Wilayani Arumeru , amesema kiasi cha shilingi 21,700,000/= zimekabidhiwa kwa Wananchi 7 .
Mtui amefafanua kuwa katika fedha hizo kiasi cha Sh.7,500,000 kimekabidhiwa kwa Waalimu 6 wa shule ya Sekondari Mariado ambao ni, Mwl.Abdallah Marambo, Mwl. Ezekiel Mwaipopo,Mwl.Andrew Mike, Mwl.Samson Hamza,Mwl.Christina Lekashu na Mwl.Ellen A. Lomau ikiwa ni mishahara yao ambayo hawakulipwa na mwajiri. Pia kiasi cha Tshs. 14,000,000/= kimekabidhiwa kwa Emmanuele Kilembe ambaye alidhulimiwa katika mauzo ya gari lake kinyume na mkataba wa mauziano.
Aidha Mtui ametoa Wito kwa wananchi kuendelea kuiamini TAKUKURU na endapo wanamalalamiko ambayo wanasadiki ni malalamiko ya kweli, wasisite kufika TAKUKURU na kama ilivyo Ada, TAKUKURU itayafanyia kazi na kuhakikisha wanapata haki yao.
Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo Ndg.Jerry Muro amesema Serikali haitamfumbia macho yeyote anayewadhulumu Wananchi ambapo amemwagiza Mkuu wa TAKUKURU Wilaya hiyo kumkamata mtu mmoja ndani ya masaa 48 anayedaiwa kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kuuza ardhi kwa mtu zaidi ya mmoja.
Muro amewaonya wanaofanya biashara ya mikopo kinyume na taratibu kwani wamek uwa wakiwanyanyasa wananchi kwa mikopo yenye riba kandamizi sambamba na kuchuk ua vitambulisho vya taifa vya wananchi hao. "ni muhimu kusajili biashara ili iwe halali na kufanyika kwa kuzingatia taratibu"amesisitiza Muro.
Wananchi waliopata haki kwa kukabidhiwa fedha zao wameishukuru Serikali kutetea haki za wanyonge ambapo Mwl. Abdalah Malambo ameushukuru uongozi wa Wilaya na kukiri kunufaika na sera ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufulu kujali wanyonge .
Emmanuel Kilembe ambaye amekabidhiwa Tshs. 14,000,000/= kama mauzo ya Gari lake amesema amefarijika sana na utendaji wa awamu ya tano kwani neno hapakazi tu linatekelezwa.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro (kulia) akikabidhiwa fedha na Ndg.Deo Mtui ambaye ni Afisa TAKUKURU Wilayani humo kiasi cha Tsh.Milion 21,700,000 kwaajili ya kuwakabidhi wanachi 7 waliodhulumiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru (kulia) akimkabidhi Ndg.Emanuel G. Kilembe Tshs. 14,000,000/= alizozulumiwa kwenye mauzo ya Gari lake.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru (kulia) akimkabidhi Mwl. Abdalah Malambo mishaara aliyokuwa hajalipwa na mwajiri wake.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akimkabidhi Mwalimu mishaara aliyokuwa hajalipwa na mwajiri wake.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akimkabidhi Mwalimu mishaara aliyokuwa hajalipwa na mwajiri wake.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akimkabidhi Mwalimu mishaara aliyokuwa hajalipwa na mwajiri wake.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa