Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru ni miongoni mwa wanufaika wa Shilingi Milioni 79,783,184 zilizookolewa mwezi Disemba 2020 naTaasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa TAKUKURU .
Sabas Salehe ambaye ni Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha wakati wa zoezi la kukabidhi fedha katika ofisi za TAKUKURU Wilaya ya Arumeru, Amewaambia Wanahabari katika Sh.Milioni 79 .7 zilizookolewa kiasi cha Sh. 27,327,884 ambazo ni fedha za Kodi na tozo za ushuru wa huduma Vibali vya ujenzi zilizohujumiwa ni za Halmashauri ya Meru na kiasi lilichobakia ni michango ya Wafanya kazi taasisi binafsi ambazo hazikuwasilishwa NSSF, fedha za vyama vya Ushirika ziluzohujumiwa na fedha za wananchi waliodhulumiwa na Wananchi wenzao na Taasisi.
Aidha Salee ametoa Wito kwa Wananchi wakiwemo watumishi wa Umma kujiepusha na Vitendo vya rushwa sambamba na jamii kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo kwa kutoa taarifa zinazohusiana na vitendo vya rushwa .
Salehe amesema katika kutokomeza vitendo vya rushwa katika Mkoa wa Arusha Taasisi hiyo imetenga siku ya Jumatano ya kila mwisho wa mwezi kuwa Siku maalum ya kupokea na kusikiliza malalamiko mbalimbali ya wananchi yanayohusu vitendo vya rushwa.
Naye Mkuu wa TAKUKURU Wilayani Arumeru Ndg.Deo Mtui amesema kwa kipindi cha miezi 6 taasisi hiyo imeokoa zaidi ya shilingi Milioni 300 ambazo zimekabidhi kwa awamu tofauti.
Mtui amefafanua kiasi hicho ni fedha kutoka kwa waliokwepa tozo na kodi mbalimbali,Waajiri wa Taasisi binafsi ambao hawakuwalipa Mishaara ya wafanyakazi, Waajiri wasio wasiowasilisha michangi ya wafanya kazi kwenye mifuko ya Jamii,na fedha nyingi ni fedha za wananchi waliodh ulumiwa na wananchi wenzao au Taasisi.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amepongeza kasi ya utendaji wa TAKUKURU wilayani humo katika kutimiza azma ya Mhe Rais ya kuhakikisha wananchi wanyonge wanapata haki bila kuonewa.
Muro amewataka Wale wote wanaojihushisha na maswala ya Rushwa Wilayani humu kuacha mara moja kwani Rungu la TAKUKURU litawafikia mahali popote walipo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Julius Ndyanabo ambaye pia ni mweka hazina wa Halmashauri hiyo amesema fedha zilizopatikana zitatumika kutekeleza shughuli za maendeleo kwa mujibu wa bajeti.
(Kulia) Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro akimkabidhi Ndg.Julius Ndyanabo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Fedha kiasi cha Sh.27,327.884.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha Sabas Salehe akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi fedha zilizookolewa na TAKUKURU Mwezi Disemba.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi fedha zilizookolewa na TAKUKURU Mwezi Disemba.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru Ndg. Deo Mtui akizungumza wakati zoezi la kukabidhi fedha zilizookolewa na aasisi hiyo Mwezi Disemba.
Mwekahazini wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Julius Ndyanabo akizungumza baada ya kukabidhiwa na TAKUKURU Sh.27,327.884 za Halmashauri hiyo.
Wananchi walionufaoka na sh.79,783,184 zilizookolewa na TAKUKURU Mwezi Disemba 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akikabidhi michango ya wafanyakazi iliyomuwa haijalipwa na waajiri kwashirika la NSSF.
Wananchi walionufaoka na sh.79,783,184 zilizookolewa na TAKUKURU Mwezi Disemba 2020.
Wananchi walionufaoka na sh.79,783,184 zilizookolewa na TAKUKURU Mwezi Disemba 2020.
Wananchi walionufaoka na sh.79,783,184 zilizookolewa na TAKUKURU Mwezi Disemba 2020.
Wananchi walionufaoka na sh.79,783,184 zilizookolewa na TAKUKURU Mwezi Disemba 2020.
Wananchi walionufaoka na sh.79,783,184 zilizookolewa na TAKUKURU Mwezi Disemba 2020.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa