Idadi ya Mifugo (Ng'ombe)iliyopo kwenye Halmashauri ya Meru yapungua, hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Mifugo kwenye Halmashauri hiyo Dkt.Amani Sanga amesema "Makadirio ya idadi ya Ng'ombe kwa mwaka 2011 yalionesha kuwa kwenye Halmashauri ya Meru kuna idadi ya ng’ombe wa asili 151,878, ng'ombe wa maziwa 83,346 jumla 235,224 tofauti na uhalisia tunao ubaini kwenye zoezi hili la upigaji chapa mifugo idadi hiyo kupungua kutokana na uhaba wa maeneo ya malisho nakusababisha wafugaji wengi kuhamishia mifugo yao kwenye wilaya zenye maeneo ya malisho pia baadhi ya wafugaji wamebadili shughuli za Kiuchumi kwa kua wakulima na wafanyabiashara"
Dkt.Sanga ameeleza kua idara yake imejipanga kuhakikisha zoezi la upigaji chapa Ng'ombe litakamilika kabla ya tarehe 01 Februari 2017 kwa kujigawa kama timu na kutoa hamasa kwa wafugaji wote kushiriki zoezi hili kutokana na taratibu zilizopangwa kwenye kila kijiji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Christopher J. Kazeri amewataka wataalamu wanao fanya kazi ya upigaji chapa Mifugo kuhakikisha Ng'ombe wote waliopo kwenye Halmashauri hiyo wanapigwa chapa kabla ya Muda wa ukomo .
Aidha zoezi hilo ya upigaji chapa linaloendelea kwenye Halmashauri ya Meru na kwa leo limefanyika katika Kata ya Ngabobo ambapo jumla ya Ngombe 1881 wamepigwa chapa hivyo kupeleke idadi ya Ng'ombe wote walio pigwa chapa kwenye Halmashauri hiyo kufikia elfu 14,055
Picha za tukio hilo
Mkuu wa idara ya Mifugo Dkt. Amani Sanga wakati wa zoezi la upigaji chapa kwenyekijiji cha Oltepesi kilichopo Kata ya Ngabobo.
Afisa mifugo wa Kata ya Ngabobo Ramadhani Maadili akichukua takwimu toka kwa wafugaji wa kijiji cha Oltepesi Kata ya Ngabobo wakati wa zoezi la upigaji chapa..
Afisa Mifugo Asanterabi Urasa akipiga chapa ng'ombe wa kijiji cha Oltepesi Kata ya Ngarenanyuki
Dkt.Charles Msigwa akipiga chapa ng'ombe wa kijiji cha Oltepesi Kata ya Ngarenanyuki
Alama wanaowekewa Ng'ombe wasio wa maziwa ikiwa na maana ya, T -inamaana ya Tanzania. MERU inamaana ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru na 56 ni namba inayotambulisha kijiji cha Oltepesi, kwani kila kijiji kianamba maalumu kwenye zoezi la upigaji chapa,Kwa Halmashauri ya Meru thamani na ubora wa Ngozi ya Ngombe ni jambo linalo zingatiwa kwa kuhakikisha chapa zinapigwa sehemu ya salama.
Kundi mojawapo ya makundi mengi ya Ngombe likielekezwa eneo la kupigia chapa
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa