Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani wakati akizungumza na
Maelfu ya Wananchi waliojitokeza eneo la Usa-River Wilayani Arumeru,amesema nchi ya Tanzania ipo Imara katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya Kisiasa ambapo amebainisha siasa sio uadui bali ni kuleta changamoto zilizopo ili zitatuliwe.
Mhe.Dkt Samia amewahakikishia wananchi Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inawaletea wananchi wake maendeleo kwa kutatua changamoto zinazowakabili ambapo ametangaza neema kwa wananchi watakaopisha eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kulipwa fidia ya Bilioni 11 ili waweze kupata makazi mengine " tumekua na kikao cha ndani na mawaziri hapa Arusha, wamepikwa wakapikikaa na wanakwenda kufanya kazi za wananachi" amesema Samia
Awali akifafanua changamoto ya miundombinu ya Barabara iliyotolewa Mhe.John Pallangyo,Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Naibu Waziri wa Ujenzi,Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kwa Wilaya ya Arumeru barabara ya Arusha -Tengeru hadi Mbuguni mkandarasi anakamilisha michoro ili iweze kujengwa Kwa kiwango cha lami katika bajeti zinazokuja na kwa changamoto ya barabara za vijijini zimeelekezwa TARURA kwa utekelezaji.
Naye ,Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande amesema kuhusu mishahara ya wafanyakazi zaidi ya 500 wa Kiliflora wanaodai fedha za mashamba ya maua alisema madai hayo yanafanyiwa kazi na ndani ya mwezi huu jambo lao litakuwa limepatiwa ufumbuzi huku uwekezaji wa mashamba ya Kiliflora yatapelekwa wizara ya Kilimo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Emmanuela Kaganda alisema wilaya hiyo itasaidiana na Halmashauri katika kilimo kupitia asilimia kumi zinazotolewa kwaaajili ya kusaidia vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Arumeru Kazi Iendelee....
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa