• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

TARATIBU ZA UBORESHAJI WA KITUO CHA AFYA USA-RIVER KITAKACHO WAHUDUMIA WATU WASIOPUNGUA ELFU 13 WAANZA

Imewekwa: January 9th, 2018

Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru  Timotheo Mzava amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha milioni 500 kwa ajili ya uboreshaji wa kituo  cha Afya  cha Usa-River kwa lengo la kusogeza huduma karibu na Wananchi pia kuviboresha vituo vya Afya kuwa na hadhi ya vituo vya Afya.

Mzava amesema  fedha hizo zitatumika kujenga miundombinu kwenye kituo hicho cha Afya ikiwa ni ujenzi wa jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto, maabara, jengo la kuhifadhia maiti, nyumba ya mtumishi, Jengo la utawala ,kichomea taka  pamoja na ukarabati wa majengo yaliyopo, pia amewataka wananchi kushiriki  kuchangia ujenzi huu ikiwa ni pamoja na  nguvu kazi.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Meru kilichopo kituo hicho cha Afya  Christopher J. Kazeri ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo kiasi cha Milioni 500  kwa ajili ya uboreshaji wa Kituo cha Afya Usa-River kwani kwenye Bajeti ya Halmashauri  hiyo haikwepo,  pia amewasihi wananchi kuitikia wito na kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano kwa kuzingatia muda .

Wananchi waliohudhuria mkutano huo wamesema wapo tayari  kushiriki na kumiliki mradi huo wa uboreshaji wa kituo cha Afya ikiwa ni baada ya kuzingatia ushauri  uliotolewa na  Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru wa kuchagua wawakilishi 10  wanaotakiwa, ambao ni  waadilifu, waaminifu, wakweli na wenye moyo wa kufanya kazi hiyo ya kujitolea.  Pia wananchi hao wameishukuru Serikali kwa kuwezesha uboreshaji wa kituo hicho cha Afya   

Mganga mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt. Cosmas Kilasara amewasihi wananchi kumiliki kituo hicho cha Afya Usa-River kwa kukitumia  pamoja na kulinda miundominu ya kituo hicho.

Daktari msimamizi wa kituo hicho cha Afya Usa-River Elinasi E. Nyari amesema kituo hicho kitakapo kamalika kitaweza kuwahudumia watu  Zaidi ya 13,320, hivyo itapunguza msongamano kwenye Hospitali za Wilaya na Mkoa, pamoja na kupunguza  Vifo vya Mama na Mtoto

    Wawakilishi wa wananchi  wa  Kata yaUsa-River kutoka vitongoji vyote vinavyounda Kata hiyo watakao shiriki kwenye uboreshaji wa kituo cha Afya  Usa-River


(wa kwanza kulia) ni Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava,katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru ,Christopher J. Kazeri na wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Cosmas Kilasara waki jadiliana jambo wakiti  wa mkutano wa wananchi wa Kata ya Usa-River.




Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa