• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

TASAF YABADILI MAISHA YA WANANCHI WA HALMASHAURI YA MERU.

Imewekwa: June 28th, 2019

Walengwa wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF)  Halmashauri ya Meru,Wilayani Arumeru wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuweka akiba na kutunza kumbukumbu kwa vikundi kutoka Kijiji cha Ngurudoto na Ngyeku, wameishukuru Serikali kwa kuwatoa katika hali duni ya maisha  kupitia malipo ya ruzuku ya  fedha kila mwezi toka mwaka 2015 hadi sasa ambapo  wanaweza  kupata mahitaji muhimu kama chakula ,mavazi ,kusomesha watoto na wengi wao wameweza kuanzisha miradi ya ufugaji ,kilimo,biashara ndogo ndogo pamoja na kujenga nyumba.

Walengwa hao  wamesema mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku mbili jana na leo, yalikuwa muhimu kwani wameshapewa vitendea kazi ambavyo ni nyaraka mbalimbali na sanduku la kuhifadhia fedha hivyo walikua hawajapata uwelewa wa kina  ambao utawasaidia kuendesha vikundi ,kuweka kumbukumbu,taratibu za kukopa na uwekaji akiba. 

Christina Mbise ambaye ni mlengwa na mwanakikundi wa kikundi cha Agape amesema TASAF imekuwa mkombozi kwake kwani mbali na kuwa maskini na kuingizwa kwenye TASAF akiwa mjane kwa kipindi cha miaka hii 3 aliweza kutumia ruzuku ya fedha anazolipwa na TASAF  kwa matibabu madogo dogo ya mtoto wake ambaye ni mlemavu wa ubongo   pia waliweza kupata mahitaji ya chakula na mavazi.

Christina amesema hakuishia kutumia ruzuku hizo kwa mahitaji madogo bali alijiingiza kwenye shughuli za kiuchumi kwa kufuga mbuzi na badae alimuuza akahamia kwenye kukuza vifaranga vya kuku ambavyo baada ya kukua aliviuza na kupata  faida ya sh.400,000 ambapo aliamua kutumia kiasi cha fedha hizo  kumpeleka mwanae mlemamu shule ya ufundi na kiasi kingine anajishughulisha na biashara ndogondogo.

Christina amewaomba wadau wa maendeleo kumsaidia mwanae huyo ili apate matibabu zaidi na makazi kwani mara nyingi huanguka na kuzimia hivyo kuwa kero kwa majirina wengine katika nyumba ya kupanga anayoishi."nilijitahidi nikanunua kiwanja kidogo lakini nimegundua kipo kwenye mkondo wa maji"ameeleza Christina

Aidha Mafunzo hayo ya kuvijengea uwezo wa kuweka akiba na kutunza kumbukumbu kwa vikundi vya walengwa wa TASAF yalianza kwa  kuwajengea uwezo wa kuvifundisha vikundi wawesheshaji ngazi ya wilaya kwa siku 3 tarehe  tarehe 25,26,27 Juni 2019 ambapo kwa sasa wataendelea kutoa mafunzo kwa vikundi vyote vya walengwa wa TASAF vilivyobaki ikiwa  mafunzo kwa Vikundi 7 Kijiji cha Ngyeku na Vikundi 11 katika Kijiji cha cha Ngurudoto yamekamilika.

Ikumbukwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru yenye Vijiji  90 ,Vijiji 47 vipo katika mpango wa kunusuru kaya maskini ,na Vijiji 20 katika Vijiji hivi 47 vina  jumla ya vikundi 122 vyenye wanachama 1732  kati yao wanawake ni 1544 na wanaume 188,vinatarajiwa kupewa mafunzo haya.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Mwl.Julius Myovela akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Amani katika Kijiji cha Ngyeku.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Antipas Massae akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Upendo Kati katika Kijiji cha Ngurudoto.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Ndg.Geturde Mkubwa akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha  Mwema  katika Kijiji cha Ngurdoto.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Sheila Mrogoro akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Umoja katika Kijiji cha Ngyeku.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Ndg.Florence Saria  akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Agape  Kijiji cha Ngyeku.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Spora Mtali akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi chakatika Kijiji cha Ngyeku.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Donata Minde akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Upendo katika Kijiji cha Ngyeku.


Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Elipokea Nassary  akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Tumaini  katika Kijiji cha Ngyeku.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Fatuma Kafuku akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Faraja katika Kijiji cha Ngyeku.


Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya ,Ndg. Mariana Mkiramwene  akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Baraka  katika Kijiji cha Ngyeku.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Anna Nduguru akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Betheli katika Kijiji cha Ngurdoto.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Lea Leina akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Amani katika Kijiji cha Ngurudoto.


Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya clementina Mbise (mwenye sweta jeusi)na Esta Mbwana (sweta jeupe ) wakitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha  katika Kijiji cha Ngurudoto.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Mary Kiondo  akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Amani katika Kijiji cha Ngurdoto.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Joyce Mruge akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Neema katika Kijiji cha Ngurudoto.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Digna Masawe akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Ndenigwa katika Kijiji cha Ngurdoto..

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Eunice Obed(mwenye sweta nyeusi) akitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Upendo katika Kijiji cha Ngurdoto.

Mwezeshaji Ngazi ya Wilaya Ndg.Agnesi Mbiseakitoa mafunzo ya uwekaji akiba na utunzaji kumbukumbu  kwa wanakikundi cha Tumaini  katika Kijiji cha Ngurudoto.


Kiongozi wa wawezeshaji  wa TASAF Ngazi ya Taifa Ndg.Hosea  Mwankusye  akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo katika kijiji cha Ngyeku,wa kwanza kulia kwake ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ngyeku  Ndg.Elibariki Mungure, na wa pili Kulia kwake 

Mfatiliaji wa TASAF Halmashauri ya Meru Judith Masika Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara baada ya mafunzo katika  kijiji cha Ngyeku.

Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Meru ,Ndg.Boniface Mwilenga baada ya mafunzo katika  kijiji cha Ngyeku

mwezeshaji  wa TASAF ngazi ya taifa Hamza Seleman kwenye mkutano wa hadhara baada ya mafunzo katika  kijiji cha Ngurudoto.

Christina Mbise ambaye ni mlengwa na mwanakikundi wa kikundi cha Agape akishuhudia namna TASAF ilivyombadilishia maisha.




Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa