Baadhi ya Walengwa wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Meru waishukuru Serikali kwani kupitia mradi wa TASAF III wamepata ujasiri wa kushirikiana na jamii tofauti na awali, ambapo walipoteza furaha kwa kushindwa kushirikiana na jamii kwenye shughuli na matukio ya pamoja kutokana na hali zao kuwa duni kiasi cha kushindwa kuwa na mavazi .
Ikiwa ni kipindi cha utoaji wa malipo kwa. kipindi cha malipo Julai /Agusti 2022 ambapo TASAF imetoa Zaidi ya Milioni 306 kwaajili ya malipo kwa walengwa elfu 6,797 pamoja na usimamizi, Elieka Mbise ambaye ni mnufaika wa TASAF, amesema alikua akiona haya kujumuika na kinamama wenzake kutokana na uchakavu wa mavazi "TASAF imetutoa mbali nilikuwa sina Kitenge hata kimoja kukiwa na shughuli yoyote nashindwa kujumuika na wenzangu"ameeleza Elieka
TASAF imekuwa na manufaa makubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru mbali kutoa malipo kwa walengwa, imekuwa ikitoa fedha kwaajili ya miradi ya Maendeleo ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita 2021/2022 TASAF ilitoa zaidi ya milioni 385 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika sekta ya Elimu ,afya,barabara nk na kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 ulioanza Julai 2022 imetoa Milioni 391.87 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Hakika Meru tunajivunia TASAF KWA MAENDELEO
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa