Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg. Emmanuel J. Mkongo amesema kuwa zoezi la upigaji kura Jimboni humo limekuwa na mafanikio makubwa kutokana wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kusubiri matokeo katika makazi yao "Uchaguzi ni mchakato mpaka majira haya ya saa 10:00 jioni zoezi la upigaji kura limekamilika na kwa sasa zoezi linaloendelea ni kuhesabu kura na kuzijumlisha ili kutangaza matokeo" ameeleza Mkongo.
Katika uchaguzi huu Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani Jimbo la Arumeru Mashariki lilikuwa na vituo 521 vya kupiga kura katika Kata 26 .Aidha, idadi ya wapiga kura jimboni humo ni 194 ,367.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa