Mapema hii Leo Timu ya Uhamasishaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Halmashauri ya Wilaya ya Meru ikiongozwa na Mwenyekiti Danieli Nanyaro imefika katika Soko la TENGERU kuhamasisha Wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27. 2024 na kuhamasisha ushiriki wa wananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura kuanzia Tarehe 11-20 mwezi Oktoba 2024.
Aidha Timu ya Hamasa imetoa Elimu kwa wananchi na kugawa vipeperushi vinavyoonyesha Utaratibu mzima unaohusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi Jitokeze kushiriki Uchaguzi "
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa