Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru Marcel Itambu amewataka walimu kutoridhika na matokeo waliyonayo na badala yake kukaza Buti ili kuleta matokeo mazuri zaidi.
Itambu ameyasema hayo Leo katika tamasha la kuwapongeza Walimu Shule za Sekondari na kutoa Motisha kwa Walimu na Shule zilizofanya vizuri katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Sasa niwaombe nyie mliopata zawadi Leo na hata ambao hamjapata zawadi, uwe una matokeo mazuri au yasiyo ridhisha, msiende kubweteka na msiridhike na matokeo mliyonayo tunapaswa kukaza kuongeza bidii ili tuwe na matokeo bora kila wakati. Tumieni mbinu zote mlizonazo za ufundishaji kuhakikisha ufaulu unaongezeka mashuleni" amesema Itambu.
Tamasha hilo la kutoa motisha limefanyika Leo Tarehe 25 Julai 2024 na kuratibiwa na Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa