Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda amewataka Watendaji wa Kata katika Halmashauri ya Meru kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu kuzingatia masuala ya lishe ili kufikia maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Kaganda amesema hayo leo katika kikao cha Tathmini ya Lishe kilichofanyika katika Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa mbalimbali ya utekekelezaji wa shughuli za lishe Idara ya Afya kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024.
Aidha, Kaganda ameipongeza Halmashauri chini ya Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Zainabu J. Makwinya, Wataalamu wa Afya, Watendaji wa Kata na Vijiji kwa utekelezaji mzuri wa afua za Afya.
Vilevile, Mhe. Kaganda amesisitiza suala la wanafunzi kupata chakula shuleni ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
"Kama tutajenga majengo mazuri na kuweka miundombinu yote lakini tukashindwa kuzingatia suala la lishe kwa watoto wetu ni kazi bure" amesema Kaganda. Hata hivyo, amesisitiza kupitia wadau mbalimbali kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu ya kuzingatia mlo kamili na lishe bora katika jamii zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa