katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kumekuwa na ongezoko la asilimia za ufaulu kutoka asilimia 75 mwaka 2017/2018 hadi asilimia 86 mwaka 2018/2019 kwa upande wa elimu Msingi na kwa elimu Sekondari kumekua na ongezeko la ufaulu madarasa ya mitihani kwa kidato cha nne ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 85.65 mwaka 2017/2018 hadi asilimia 86.53 mwaka 2018 pia kidato cha Sita ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 98.75 kwaka 2017/2018 hadi 98.75 mwaka 2018/2019 ambapo shule ya Sekondari Kisimiri ilishika nafasi ya pili Kitaifa na nafasi ya kwanza Kimkoa.
Hayo yamejiri wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Halmashauri hiyo kupitia taarifa ya uwajibikaji iliyosomwa na Afisa Mipango Bw.Maarufu Mkwaya imeeleza kuwa Halmashauri hiyo kupitia mapato yake ya ndani kwa mwaka wa fedha 2018/2019 imetoa Tsh milioni 63,617,797.73 kwaajili ya ununuzi wa bati 735,mifuko ya Saruji 769 na madawati 600 kwa shule za Sekondari pia kupitia mfuko wa Jimbo jumla ya Tsh135,380,000 zilitumika kununua bati 1008 kwaajili ya kuwezeka vyumba vya madarasa na mifuko ya Saruji 1280 na upande wa Elimu Msingi Serikali kupitia mradi wa EP4R Serikkali kuu ilitoa jumla ya TSH 293,200,0 00 ambayo ilitumika kujenga na kukamilisha vymba 20 vya madarasa na matundu ya vyoo 12 katika shule 18.
Ikumbukwe kuwa kupitia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundisha kupitia fedha za Serikali kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Meru umeleta mafanikio makubwa na kuifanya Halmashauri hiyo kung'ara kwa kushika nafasi ya tatu Kitaifa naya kwanza kimkoa katika matokeo ya mtiani wa taifa kidato cha Nne na cha pili mwaka 2019.
Aidha katika Mkutano huo Nelson Mafie ambaye ni diwani wa Kata ya Malula alichaguliwa kwa mara nyingine kuwa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja 2019/2020 sambamba na kuchagua na kuunda kamati tatu za kudumu za Halmashauri hiyo ambazo ni kamati ya elimu, afya na maji ambayo itaongozwa na Mwenyekiti Gadiel Mwanda diwani kata ya Imbaseni , kamati ya uchumi ujenzi na mazingira itaongozwa na mwenyekiti Underson Pallangyo Diwani Kata ya Maji ya chai ,Kamati ya Maadili itaongozwa na Yona Kaaya Mhe. Diwani Kata ya Maroroni.pia kamati ya fedha mipango na utawala itaongozwa na Willy Njau Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Willy Njau wakati wa ufunguzi wa mkutano huo aliwaelekeza wajumbe kuzingatia kanunu za kuendeza vikao ili kuweza kujadili,kushauri na kufanya maamuzi kwa maslai mapana ya Halmashauri hiyo ikiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika baaada ya Msimamizi wa ulinzi na usalama Wilaya ya Arumeru kusitisha vikao katika Halmashauri hiyo tarehe 28 Agusti 201 9.wakati wa mkutano wa baraza hilo kuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Willy Njau akizungumza wakati wa mkutano wa mwaka wa Baraza la Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg. Emmanuel J. Mkongo wakati wa mkutano wa mwaka wa Baraza la Halmashauri hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mhe.Nelson Mafie wakati wa mkutano wa mwaka wa Baraza la Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Yona Kaaya Mhe. Diwani Kata ya Maroroni
Mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na maji Gadiel Mwanda diwani kata ya Imbaseni
Mwenyekiti wa kamati ya uchumi ujenzi na mazingira, Underson Pallangyo Diwani Kata ya Maji ya chai
Waheshimiwa madiwani wakati wa mkutano wa mwaka .
Waheshimiwa madiwani wakati wa mkutano wa mwaka
Waheshimiwa madiwani wakati wa mkutano wa mwaka
Diwani wa kata ya Kikwe akichangia wakati wa mkutano wa mwaka wa baraza.
Diwani wa kata ya Mbuguni akichangia wakati wa mkutano wa mwaka wa baraza.
Diwani wa kata ya Makiba akichangia wakati wa mkutano wa mwaka wa baraza.
Waheshimiwa madiwani wakati wa mkutano wa mwaka
Wakuu wa Idara na Vitengo,Wataalam wakati wa mkutano wa baraza la mwaka.
Wakuu wa Idara na Vitengo,Wataalam wakati wa mkutano wa baraza la mwaka.
Wakuu wa Idara na Vitengo,Wataalam wakati wa mkutano wa baraza la mwaka.
Wakuu wa Idara na Vitengo,Wataalam wakati wa mkutano wa baraza la mwaka.
Wakuu wa Idara na Vitengo,Wataalam wakati wa mkutano wa baraza la mwaka.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa