Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanuel Mkongo ameridhishwa na upatikanaji wa dawa katika Kituo cha afya Mbuguni alipo kitembelea na kuzungumza na watumishi wa kituo hicho.
Mkongo amesema upatikanaji wa dawa lazima uendane na matumizi sahihi hivyo amewataka wasimamizi wa vituo vya kutoa huduma za afya kwenye Hamashauri hiyo kuagiza dawa zinazohitajika kwa wakati sambamba kudhibiti matumizi ya dawa kwa ujazaji wa fomu za huduma za dawa (BIN GARD),"sitegemei mwananchi kukosa dawa yoyote kwenye kituo cha Afya" Amesisitiza Mkongo.
Mkongo ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizotolewa na watumishi wa kituo cha Afya Mbuguni.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake Dkt.Hakimu Kaluse amempongeza mkurugenzi kwa Kuwatembelea kwani wanaamini changamoto ya upungufu wa watumishi na uchakavu wa baadhi ya miundombinu zitafanyiwa kazi.
Mkurugenzi Mkongo toka aripoti Halmashauri ya Wilaya ya Meru tarehe 20 Agosti 2018 amekua akikutana na watumishi wa kada mbalimbali kwa lengo la kusikiliza changamoto walizo nazo na kuzifanyia kazi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa Majukumu .
Kikao kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Watumishi wa kituo cha Afya Mbuguni.
Mkurugenzi Mkongo akikagua chumba cha kuhifadhia dawa katika kituo cha afya Mbuguni.
Watumishi wa Kituo cha Afya Mbuguni wakati wa kikao na Mkurugenzi Mkongo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa