Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kituo hicho ,mwenyekiti wa kamati hiyo ya ujenzi Allen M. Mwenda amesema wanaridhishwa na ujenzi unaoendelea kwani changamoto iliyokuwepo ni ya vifaa na kwa sasa vifaa vyote vinavyohitajika vipo na mafundi wanaendelea na ujenzi pia amefafanua kuwa ujenzi huo umekua fursa ya ajira kwa vijana ,wanawake na wananchi wengine hivyo nguvu kazi ipo ya kutosha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher J. Kazeri ameeleza kuwa usimamizi na ufuatiliaji wa ukaribu unafanyika kwenye ujenzi na uboreshaji wa kituo hicho cha Afya na utakamilika kabla ya tarehe ya ukomo iliyotolewa (31 Mai 2017 )na wananchi kupata huduma .
Aidha Mkurugenzi Mtendaji bwana Kazeri amewahimiza wataalamu wanaosimamia ujenzi huo kuzingatia ubora kwa kueleza kuwa lengo la kutumia Force Account ni kupunguza gharama,kuondoa urasimu na kuharakisha ujenzi huo kukamilika mapema.
Fedha kiasi cha shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kuendeleza kituo kituo cha afya Usa – River kwa lengo la kuboresha huduma za afya na kupunguza na kuondoa vifo vya mama na mtoto
Mpaka sasa shughuli zilizofanyika kwenye uboreshaji wa kituo hicho ni Ujenzi wa Majengo ya maabara na nyumba ya Mtumishi yaliyofikia hatua ya upauzi pamo pia ujenzi wa misingi ya majengo mengine unaendelea .
ujenzi wa jengo la nyumba ya mtumishi
ujenzi wa jengo la maabara
ujenzi msingi wa jengo la wodi ya mama na mtoto
ujenzi msingi wa jengo la upasuaji
(wakwanza kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher J. Kazeri akiteta jambo juu ya ubora wa ujenzi wa msingi wa jengo la jengo la kuhifadhia maiti,
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa