MERU DC YAPONGEZWA KATIKA MIRADI YA SEQUIP NA BOOST
Imewekwa: February 21st, 2024
Halmashauri ya Meru imepongezwa kwa utekelezaji wa ujenzi wa Miradi ya SEQUIP na BOOST na kwamba imekuwa mfano kwa kuhakikisha Miradi hiyo imekamilika na kufuata maelekezo yote yaliyotolewa katika kutekeleza miradi hiyo.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya SEQUIP na BOOST kutoka Benki ya Dunia, OR - TAMISEMI, Wizara ya ELimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Katibu Tawala Msaidizi Elimu Mkoa wa Arusha imekagua Miradi hiyo na kufurahishwa jinsi ambavyo Halmashauri imetekeleza miradi hiyo.
Aidha katika ziara hiyo, Mratibu Msaidizi wa Miradi BOOST Reuben Swilla ameshauri Walimu Wakuu wahakikishe wanasimamia vizuri taaluma ya wanafunzi ili shule hizo ziwe na ufaulu mzuri kama ambavyo majengo ni mazuri na yanavutia.
Hata hivyo, Mtaalamu wa Masuala ya Manunuzi kutoka Benki ya Dunia Fredrick Nkya amepongeza kazi nzuri iliyofanyika na ameshauri Halmashauri ianze kuangalia kuboresha mazingira ikiwa ni pamoja na kuweka Uzio katika shule, kuweka vibao vya masuala ya kupinga ukatili na kufanya "Landscaping".