UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA ROBO PILI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.
Imewekwa: February 24th, 2024
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wamefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja ukamilishaji wa wa jengo la kufulia, miundombinu ya vyoo na maji katika kituo cha Afya Mareu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru imepokea kiasi cha shilingi Milioni 50,000,000.00 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa kichomea taka, Shimo la kutupa Kondo,Shimo la kutupa majivu, kinawia mikono, stendi ya tenki na vyoo matundu matano.
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Meru imechangia jumla ya shilingi 52,000,000.00 ambapo fedha hizo zimewezesha ujenzi wa jengo la kufulia ambalo linaenda sambamba na la huduma za Afya ya mama na mtoto.
Jengo hilo linauwezo wa kutoa huduma kwa wananchi wapatao 7003 na majengo ya maabara ya chumba cha mionzi yanatarajia kutoa huduma kwa wananchi wapatao 12,912 na Kaya 3162 katika Kata za King'ori, Malula, Leguruki, Maruvango na maeneo ya Wilaya za jirani.