Diwani wa Kata ya Nkoarisambu Mhe.Godfrey Nassari ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya fedha mipango na UTAWALA katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru apongeza namna Halmashauri inatekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi ikiwemo utoaji wa vifaa badala ya fedha kwenye ngazi za Kata na Vijiji.
Mhe.Nassari amesema hayo wakati wa Ziara ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya alipotembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Nkoarisambu ikiwa ni Muendelezo wa ziara yake ya kutembelea miradi ya Maendeleo Kata kwa Kata.
Mhe .Nassari amefafanua kuwa upelekaji wa vifaa umeongeza tija na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi, "utoaji wa vifaa Umeondoa changamoto ya Bei kupanda pia ubora unaohitajika umekuwa ukizingatiwa"amesema mhe.Nassari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ametoa wito kwa viongozi kuhamasisha na kuwaelimisha Wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Aidha Mhe Godfrey Nassari amesema kwa sasa Wananchi wa Kata hiyo wapo kwenye mpango wa kushiriki shughuli za maendeleo kwa kugawana majukumu ambapo katika Vijiji 3 Kazi zitakazo fanyika ni ujenzi wa Choo Cha matundu 10,ukarabati wa Madarasa pamoja na ujenzi Wa Kivuko.
Kata ya Nkoarisambu ni Miongoni mwa Kata saba(7) ambazo Mkurugenzi Zainabu amefanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa miradi ya EP4R ,Miradi ya Nguvu za wananchi na michango ya wahisani,miradi ya TASAF pamoja na maboma ya mda mrefu ,ambapo aliambatana na Afisa Elimu Sekondari pamoja na Wahandisi wa Ujenzi toka Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya (nguo nyekundu),Kulia kwake ni Diwani wa Kata ya Nkoarisambuni Mhe.Godfrey Nassari pamoja na viongozi,Walimu wa Shule ya Nkoarisambu.
Jengo la maabara katika Shule ya Sekondari Nkoarisambu.
Jengo la maabara katika Shule ya Sekondari Nkoarisambu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa