Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanula Kaganda akifungua Mkutano wa wadau mbalimbali wakati wa kutambulisha Mradi wa Ujenzi na Upanuzi wa barabara ya njia nne kuanzia Tengeru hadi Usariver (NJIA PANDA YA MOMELA) barabara yenye urefu wa kilometa 11.47.
Mhe. Kaganda ameeleza kuwa lengo la kupanua barabara hizi ni kuongeza kasi ya mwendo barabarani na kurahisisha huduma kufikiwa kwa haraka bila kuchelewa.
Kaganda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo lakini pia kuboresha miundombinu ya barabara.
Ameeleza kuwa Mkoa wa Arusha umebarikiwa kwa vivutio vingi vya watalii lakini kwa Wilaya ya Arumeru ndio lango la Jiji la Arusha hivyo mradi huu wa barabara utazidi ufanya Arumeru kuwa na hadhi zaidi.
Pia, amemshukuru Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe. John Daniel Pallangyo kwa kuisemea na kuitetea Halmashauri ya Meru Bungeni hadi kupelekeza kupata fedha nyingi za miradi ya maendeleo.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa