Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewataka viongozi wa vyama vya ushirika wilayani humo wasioweza kuviongoza vyama hivyo kujiuzulu mara moja.
Mhe.Muro amesema hayo katika uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru, ambapo amesema atasimamia ushirika wilayani humo ili uweze kuimarika na kudumu.
Mhe.Muro amesikitishwa na ubadirifu wa fedha za wanachama wa ushirika kwa maslahi ya viongozi wachache kinyume na lengo la serikali kuwaunganisha wananchi pamoja ili waweze kujikwamua kiuchumi na kijamii.
Muro ameviasa vyama vya ushirika kutumia wataalamu wenye sifa ili kuleta ufanisi kama sheria namba 6 ya mwaka 2013 inavyowataka.
Akihitimisha Mhe.Muro amewapa muda wa mwezi mmoja viongozi wote wa vyama vya ushirika Wilayani Arumeru kuwasilisha taarifa za kipindi cha miaka 5 za mapato na matumizi, taarifa za mali za vyama pamoja na taarifa ya idadi ya wanachama,watumishi sambamba na mihutasari ya vikao.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Ushirika Halmashauri ya Meru ambapo uzinduzi wa jukwaa hilo umefanyika ,Ndg. Mkumbwa Mussa amesema wamejipanga vyema kuvisimamia Vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kufanya Ukaguzi wa kushtukiza mara kwa mara.
Nao wajumbe wa jukwaa la Ushirika Wilayani Arumeru wameazimia kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa ikiwa ni pamoja na kutumia wiki 3 kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya uwasilishaji wa taarifa.
lengo la uundaji wa Majukwaa ya ushirika ngazi ya Mkoa na Wilaya ni kutoa fursa kwa wanachama na wadau mbalimbali kujadili
Maendeleo na changamoto zinazoukabili ushirika na kuweka mikakati ya kutatua changamoto hizo ili kuviimarisha Vyama vya Ushirika.
Wilaya ya Arumeru ina Halmashauri mbili ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Idadi ya vyama vya ushirika Wilaya ya Arum ni 113 ikiwa ni 73 vipo Halmashauri ya Wilaua ya Meru na 40 vipo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
PICHA ZA TUKIO.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro.
(kushoto) kwa mkuu wa wilaya Arumeru ni Mwenyekiti wa Jukwaa la ushirika Mkoa wa Arusha Ndg. Wilibald Ngambeki na kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wilaya ya Arumeru Mch.Anaeli Nassari.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirika Halmashauri ya Meru Mkumbwa Mussa (kulia ) pembeni yake ni Afisa ushirika kwenye Halmashauri ya Meru Neema Munisi.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Viongozi wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika Wilaya ya Arumeru.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru,viongozi wa Jukwaa la Ushirika Arumeru na viongozi wa vyama vya ushirika.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa