Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula (mbunge)amewataka wanachi wa Kata ya Sing’isi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuwa na subra kwa kipindi cha mwezi mmoja wa utatuzi wa migogoro ya Ardhi iliyopo kwenye Kata hiyo.
Naibu Waziri Angelina Mabula amesema hayo alipo kuwa kwenye mkutano wa adhara ya wananchi uliofanyika kwenye Kata hiyo na wananchi kutoa malalamiko yao kuhusiana na migogoro ya ardhi wengi wao wamelalamikia Ardhi yenye ukubwa wa Hekari 50 na mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Yohana A. Kimuto amesema ugawanyaji wa ardhi hiyo ulifanyika kinyemela.
Naibu waziri Angelina Mabula baada ya kusikiliza malalami ya wananchi amesema mbali na jitihada mbalimbali zilizofanyika kwenye ngazi ya Mkoa na Wilaya katika kutatua migogoro ya ardhi kwenye Kata hiyo Wizara yake itaunda tume itakayofanya uchambuzi wa kina na kitaalamu wa migogoro hiyo na majibu kutolewa kwa wananchi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, nukuu “Hatuwezi kupeleka mambo haraka bila kuzingatia sheria na taratibu tukaingia kwenye hatia”.
Ikumbukwe kuwa Wizara ya Ardhi hivi karibuni ilizindua kampeni yenye lengo la kutokomeza migogoro ya ardhi mijini na vijijini iliyopewa jina la funguka kwa waziri,
Aidha utekelezaji wa Kampeni hiyo utafanyika kwa njia ya ujazaji fomu maalumu zitakazo sambazwa na wizara kwenye ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya pia utekelezaji huo utafanyika kwenye mikutano ya hadhara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi
Picha za tukio.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ya wananchi wa kata ya Sing'isi.
Kaimu mkuu wa idara ya Ardhi na Maliasili Ndg. Shairu Chuma akitoa ufafanuzi kwenye mkutano wa hadhara ya wananchi wa kata ya Sing'isi.
Diwani wa Kata ya Sing'isi Penzila Pallangyo akizungumzakwenye mkutano wa hadhara ya wananchi wa kata ya Sing'isi.
S . Akyoo akitoa lalamiko la migogoro ya Ardhi iliyopo .
Wananchi wa Kata ya Sing'isi. wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi Angelina Mabula
Wananchi wa Kata ya Sing'isi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi Angelina Mabula.
Wananchi wa Kata ya Sing'isi wakiwa kwenyemkutano wa hadhara na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo yaMakazi Angelina Mabula.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa