Kuelekea maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wanafunzi wa Shule ya Msingi Kikwe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Wilayani Arumeru waondokana na changamoto ya uchakavu wa vyumba vya madarasa baada ya Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa shilingi Milioni 60 za ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja Samani (Meza na viti 50 kwa kila darasa) shuleni hapo.
Akizundua vyumba hivyo vya Madarasa, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda
amesema Wilaya ya Arumeru inaishukuru Serikali kwani kuelekea miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Serikali ya awamu ya sita imetoa fedha nyingi katika sekta za Elimu,Afya ,Kilimo nk
Mhe.Kaganda ameipongeza Serikali ya Dkt.Samia kwani imehakikisha wanafunzi wanasoma kwenye vyumba vya kisasa vya madarasa vyenye viti na Meza, Umeme, vigae (tiles) ambapo ametoa wito kwa Walimu kusimamia utunzaji wa miundo mbinu mashuleni ili kuwa na tija zaidi.
Vilevile Mhe.Kaganda amewapongeza viongozi wote walioshiriki kusimamia ukamilishaji wa mradi wa huo, ambapo ametumia jukwaa hilo kuwakumbusha Wakulima kulima mazao ya muda mfupi kuzingatia taarifa za mamlaka za Hali ya Hewa, na kubainisha kwa Sasa mbolea inapatikana Wilayani Humo .
Mhe.Daniel Kaaya ambaye ni Diwani wa Kata ya kikwe amesema ndani ya miaka miwili wamefanikiwa kupata miradi mingi ambayo kila kijiji cha kata ya kikwe kimepata mradi.
kwa upande wao wazazi na Wanafunzi wameishukuru Serikali kutoa fedha za ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa kwani kwa Sasa wanafunzi watasoma katika mazingira mazuri na rafiki.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa