Mkurugenzi Mtendajiwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Ndg. Emmanuel Mkongo amewataka wawezeshaji wa mfuko wa kunusuru kaya maskini (TASAF) katika Halmashuri hiyo kutumia vyema mafunzo wanayopewa ya utunzaji wa kumbukumbu na fedha kuvifundisha vikundi vya wananchi wanaofadhiliwa TASAF ili waweze kujiinua kiuchumi kutumia kupitia fedha wanazopewa katika kubuni na kuanzisha miradi ya uzalishajimali.
Mkurugenzi amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa TASAF Ngazi ya Wilaya na Kata katika Halmashauri hiyo ambapo amewataka kutumia mafunzo hayo kama chachu ya kwenda kutoa elimu katika vikundi vya jamii husika vinavyo toka katika kaya maskini ili viweze kuongeza kipato na kupiga hatua kiuchumi.
Mtaalamu wa Mafunzo na Ushirikishwaji kutoka TASAF Makao makuu,Ndg.MERCY MANDAWA amesema wawezeshaji kwenye Halmashuri zote nchini wamechangia kwa kiasi kikubwa katiks utekelezaji wa TASAF kuwa rahisi ,hivyo ametoa rai kwao kutumia mafunzo hayo kuisaidia jamii kujua kutunza kumbukumbu na kuweka akiba kwa lengo la kujikwamua kutoka hali duni.
Mratibu wa TASAF katika Halmashuri hiyo Boniface Mwilenga amesema vijiji 47 kati 90 vya Halmashauri hiyo vipo katika mpango wa kunusuru kaya maskini,aidha katika vijiji hivyo 20 jumla ya vikundi 122 vyenye wanachama 1732 vimeundwa na vinajiendesha na kati yao wanawake ni 1544 na wanaume 188.
Aidha Mwilenga amesema vikundi hivyo vinajiendesha vyenyewe na vimeshapewa shajala mbalimbali likiwemo daftari la kutunza kumbukumbu na sanduku la kuhifadhia fedha, hivyo vinahitaji mafuzo ili kuboreshe utendaji wao wa Kazi.
Baadhi ya wawezeshaji wanaopata mafunzo hayo,Ester Mbwana,Agness Piter na Donatha Minde wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika kuwajengea uwezo wa kwenda kuwafundisha wanavikundi walioko katika maeneo yao kutumia fedha kidogo ili kujikwamua katika umaskini.
Mafunzo hayo ya TASAF ambayo yanafanyika katika mikoa miwili tu Nchini ,ambapo kwa mkoa wa Njombe yamekamilika na kwa Mkoa wa Arusha Arusha yanaendelea ambapo katika Halmashauri ya Meru yanafanyika kwa siku 5 katika kumbi za Halmashauri .
Ester Mbwana ni miongoni mwa wawezeshaji wanaopata mafunzo hayo .
Agness Piter ni miongoni mwa wawezeshaji wanaopata mafunzo hayo
Donatha Minde ni miongoni mwa wawezeshaji wanaopata mafunzo hayo
Kulia ni afisa ufuatiliaji wa TASAF (TMO) Judith Massika an Kulia ni Hosea Mwankusye Kiongozi wa timu ya wawezeshaji kitaifa.
wawezeshaji wa TASAF wakifuatilia Mafunzo.
wawezeshaji wa TASAF wakifuatilia Mafunzo.
Hamza Seleman ambaye mwezeshaji ngazi ya Taifa akitoa mafuzo kwa wawezeshaji ngazi ya Kata na Halmashauri
wawezeshaji wa TASAF wakifuatilia Mafunzo.
Abdallah Dokodoko ambaye mwezeshaji ngazi ya Taifa akitoa mafuzo kwa wawezeshaji ngazi ya Kata na Halmashauri.
wawezeshaji wa TASAF wakifuatilia Mafunzo.
wawezeshaji wa TASAF wakifuatilia Mafunzo.
wawezeshaji wa TASAF wakifuatilia Mafunzo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa