Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya maradhi ya Surua Rubella na Polio katika Kituo cha Afya Usa -River Halmashauri ya Meru.
Muro Ametoa wito kwa wazazi kutosubiri kuona dalili za magonjwa hayo bali wawapeleke watoto kupatiwa chanjo hiyo itawakinga na madhara mbalimbali ikiwemo kupooza ghafla.
Aidha amefahamisha kuwa zoezi la utoaji chanjo litaendelea kwa siku tano hadi tarehe 21 ambapo linawalenga watoto kuanzia umri wa miezi tisa hadi miaka mitano ambao ndio waathirika zaidi wa maradhi hayo.
Naye mganga mkuu kwenye Halmashauri hiyo,Dkt Maneno Focus amesema lengo la kampeni hiyo ni kuzuia na kupambana na maradhi yanayozuilika kwa chanjo. itakayotolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya vya kudumu 58 na maeneo 126 vya muda na malengo ni kuwafikia watoto 33136 kwa chanjo ya surua rubella na watoto 22112 kwa chanjo ya polio ya sindano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo ametoa wito kwa jamii kuona umuhimu wa zoezi la chanjo kwa mustakabali wa afya za watoto kwani huduma hiyo inatolewa bure.
Akifafanua dalili za maradhi ya Surua na Rubella mratibu wa afya ya uzazi na watoto Sikudhani Mkama, mtoto kuwa na homa kali kuchuruzika mafua macho kuwa mekundu na kumwaga machozi hivyo akina mama wawapeleke watoto kupata chanjo.
Zoezi la uzinduzi wa kampeni hiyo ya Chanjo limefanyika katika vituo vyote vya Halmash auri ya Meru
Wazazi na watoto wakati wa uzinduzi wa Chanjo.
Muuguzi akitoa maelezo kabla ya chanjo kwa mtoto wa kwanza wakati qa uzinduzi.
Mkuu wa Wilaya Meru akiwa na mtoto wa kwanza kupata chanjo ya ugonjwa wa Surua, Rubella na polio wakati wa uzinduzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Picha ya pamoja.
Uzinduzi Nkonekoli.
uzinduzi leguruki lutheran zahanati ya shirika la dini.
zahanati ya Usa Rc.
Zahati ya King'ori.
Mtendaji wa kata kimundo akizindua zoezimtendaji wa kata kimundo akizindua zoezi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa