Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Idd Kimanta amesema hatua kali za kisheria zitachikuliwa dhidi ya mtu yoyote atakaye kuwa kikwazo kwa namna yoyote kwenye zoezi la utoaji chanjo ya kinga ya Saratani ya shingo ya mlango wa kizazi inayotolewa kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi 14 kwani chanjo hiyo ni juhudi ya Serikali kutokomeza saratani hiyo kwa kizazi kijacho.
Mhe. Kimanta amesema hayo wakati wa uzinduzi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru wa chanjo ya Kinga ya saratani ya shingo ya kizazi (HPV)uliofanyika katika Hospitali ya Wilaya Tengeru ambapo ametoa agizo kwa maafisa elimu ,watendaji wa Kata na Vijiji na viongozi wote kwenye Halmashauri hiyo kuhakikisha watoto walengwa kwenye maeneo yao wanapata chanjo hiyo.
Naye mganga mkuu kwenye Halmashauri hiyo Dkt.Cosmas Kilasara ameeleza kuwa kati ya wanawake elfu 5,892 waliofanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya mlango wa kizazi mia 319 kati yao walibainika kuwa na maambukizi ya awali na mia 119 walikuwa wamepata mashambulizi makubwa ya saratani hiyo hivyo walipewa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi pia ametoa wito kwa wanawake kufanya uchunguzi mara kwa mara wa Saratani hiyo kwani huwa rahisi kutibika inapokuwa kwenye hatua za awali.
Dkt. Kilasara ameenda mbali zaidi kwa kueleza Ugonjwa huo wa Saratani ya shingo ya mlango wa uzazi (HPV) hutokana na mabadiliko ya ukuwaji wa seli kwenye mwili wa mwanamke ambayo huathiri misuli na viungo vingine na visababishi vya saratani hiyo ni pamoja na kufanya mapenzi kwenye umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,ndoa za mitara,kuzaa watoto wengi pamoja na uvutaji wa sigara.
Mratibu wa chanjo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Jonathan Mollel ametoa wito kwa wasichana kutoshiriki tendo la ndoa wakiwa na umri mdogo pia amewasihi wazazi kushiriki kikamilifu kuhakikisha watoto wao wenye umri husika wanapata chanjo hiyo ya kinga ya saratani ya shingo ya kizazi ,sambamba na wanawake kuwa na utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara.
Mmoja wa wasichana waliopata chanjo hiyo (jina limehifadhiwa) ameishukuru Serikali kwa kumtamini mwanamke kwani mwanamke anapokua salama familia huimarika.
PICHA ZA TUKIO.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Idd Kimanta akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kinga ya saratani ya mlango wa kizazi.
Mganga mkuu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kinga ya saratani ya ahingo la mlango wa kizazi.
Mmoja ya wasichana waliopata chanjo ya kinga ya saratani ya shingo la kizazi.
Wasichana walipata chanjo ya Saratani ta shingo la mlango wa kizazia wakiwa kwenye uzinduzi.
Wasichana walipata chanjo ya Saratani ta shingo la mlango wa kizazia wakiwa kwenye uzinduzi.
Wasichana walipata chanjo ya Saratani ta shingo la mlango wa kizazia wakiwa kwenye uzinduzi.
Kinamama waliowaleta watoto wak kupata chanjo mbalimbali ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya chanjo
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Wilaya Tengeru na wazazi wakiwa kwenye uzinduzi.
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Wilaya Tengeru na wazazi wakiwa kwenye uzinduzi
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Wilaya Tengeru na wazazi wakiwa kwenye uzinduzi
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Wilaya Tengeru na wazazi wakiwa kwenye uzinduzi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa