Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mohamed Mkalipa
Mapema hii Leo amefungua Semina ya Mafunzo Kwa Maafisa maendeleo ya Jamii waliopitishwa kwenye kanuni zilizoboreshwa za uundaji wa Vikundi na uandishi wa maandiko ya Miradi ngazi ya Kata.
Mhe. Mkalipa amewataka Maafisa hao kwenda kutengeneza Vikundi vitakavyowanufaisha Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kuacha kupokea maelekezo ya watu kutoka mifukoni kwani wakati huu mpaka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imejiandaa vilivyo kuhakikisha Fedha hizo zinatolewa Kwa utaratibu nakurudishwa Kwa utaratibu unaohitajika.
Aidha wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya amewasisitizia Maafisa hao kwenda kuzingatia maelekezo nakufata taratibu na kanuni kulingana na Yale watakayo fundishwa, ili kuepusha usumbufu na upotevu wa muda wakati wa kurudisha na kudai urejeshwaji wa Mikopo Kwa manufaa yawengine.
Mikopo hii Kwa Makundi haya Maalumu Vijana, Wanawake na wenye ulemavu ilisitishwa Mwaka 2023 mwezi wa 4 kwakutafuta utaratibu uliobora Kwa ajili ya ukopeshaji na kuwafikia walengwa wote wenye uhitaji ili kuleta Maendeleo ya mtanzania Mmoja mmoja. Hata hivyo, Mikopo hiyo inatarajiwa kutolewa mapema mwanzoni mwa mwezi huu Oktoba Kwa wale wote wenye sifa.
Mkalipa amewasisitizia Maafisa maendeleo ya Jamii kwenda kupeleka Elimu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakati watakapokuwa wanatoa Elimu ya ukopaji wa Mikopo hiyo ili kusaidia kupata viongozi Bora watakao leta maendeleo kwenye Jamii zinazowazunguka.
Semina hii inatarajiwa kufanyika Ndani ya Siku tano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa