Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mohamed Mkalipa amegawa vitambulisho 924 Kwa wajasiriamali wanaojishughulisha na Biashara mbalimbali ikiwa ni kwa awamu ya kwanza ya ugawaji ambapo Lengo la Halmashauri nikugawa vitambulisho 1501 Kwa wajasiriamali waliosajiliwa.
Aidha, lengo la vitambulisho hivyo ni kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili wajasiriamali katika shughuli zao za kila siku ikiwa ni pamoja na kukosa Mikopo, kusumbuliwa kuhusu kodi na swala zima la Bima. Vitambulisho hivi vitakwenda kutatua changamoto hizo.
Zoezi hili la ugawaji wa vitambulisho limefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru likiwa chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa