Shule ya Sekondari Kisimiri iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilaya ya Arumeru , ambayo ilishika nafasi ya kwanza Kitaifa katika matokeo ya kidato cha Sita mwaka 2019, imeendelea kufanya vizuri Kitaifa ambapo wanafunzi wake wa tafiti za kisayansi wameshika nafasi ya pili Kitaifa katika mashindano ya Kitaifa ya Vijana watafiti wa kisayansi yaliyofanyika Jijini Dar es salaam tarehe tarehe 01 - 02 Agosti 2019,
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisimiri Mwl.Valentine Tarimo mbele ya Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wakati Kamati hiyo ilipofika shuleni hapo kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Aidha Mwl.Valentine amefafanua kuwa katika mashindano hayo yaliyoshirikisha Shule 97 zenye wanafunzi 194, Wanafunzi wanne (4) kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri walishiriki na kuibuka washindi wa pili huku nafasi ya kwanza ikienda kwa wanafunzi toka Shule ya Sekondari Chief Dodo iliyopo Mkoa wa Manyara na nafasi ya tatu ilichukuliwa na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari St. Jude ambayo pia ipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Ushindi huo ulipelekea Shule ya Sekondari Kisimiri kushika nafasi ya pili na kutunikiwa tuzo tatu, pia wanafunzi walioshiriki walipewa medali na fedha kiasi cha sh.1,500,000 .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amepongeza juhudi za walimu, wanafunzi na wazazi katika kuinua kiwango cha elimu katika Shule ya Sekondari Kisimiri na kuhaidi kutoa ushirikiano kwa shule hiyo ili iendelee kufanya vizuri zaidi.
Aidha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango imekamilisha ziara yake kwa siku ya kwanza kwa kukagua miradi ya Ujenzi wa nyumba ya mtumishi (Mganga) katika zahanati ya kijiji cha Ngabobo, Ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Ilikirimuni, Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Shishtoni na Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Ngejusosia Kata ya Malula.
Wanafunzi Joseph Masangu na Vicent Gabriel Laizer walioshinda tuzo ya mshindi wa pili Kitaifa.
Wanafunzi Albert Muhagama and Enid Nobert walishinda tuzo Maalumu.
Wanafunzi 4 walioshiriki Mashindano wakiwa na walimu wao.
(wa pili kutoka kushoto)Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaua ya Meru Mhe.Will Njau,kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti Nelson Mafie,kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Kisimiri Mwl.Valentine Tarimo ,Wa pili kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Emmanue Mkongo kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ,afya na mazingira Elisa Mungure wakifurahia tuzo za ushindi.
Picha ya pamoja ya Kamati ya Fedha utawala na mipango , Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisimiri .
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisimiri akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujezi wa nyumba za walimu 6i in one.
Ujezi wa Mradi wa Zahanati ya kijiji cha Ngabobo.
Mhe.Diwani Kata ya Ngabobo Solomon Laizer akitoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa Mradi wa Zahanati ya Kijiji cha Ngabobo.
Ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Ilikirumuni Kata ya Ngarenanyuki.
Mtendaji wa Kijiji cha Elikirimuni Akisoma taarifa ya ujezi wa Mradi wa Zahanatiya kijiji hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meruwakati wa ukaguzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ilikirimuni.
Mwenueki wa Halmashauri akipata maelezo toka kwa mtaalamu wa Idara ya ujenzi.
Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Shishiton Kata ya Maruvango.
Wajumbe wa Kamati ya fedha ,mipango na utawala wakisomewa taarifa ya ujenzi wa kijiji cha Shishiton toka kwa Mtendaji wa Kijiji hicho.
Ujenzi wa Zahanati ua kijiji cha Ngejisosia Kata ya Malula.
Wajumbe wa Kamati ya fedha,utawala na Mipango wakikagu ujenzi wa Zahanati ya kijiji chaNgejisosia.
Diwani Kata ya Malula,ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri akitoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ngejososia.
Wajumbe wa kamati ya fedha,utawala na mipango wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Mradi wa Zahanati kijiji cha Ngejisosia.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa