Naibu Waziri wa maji Mh. Juma Aweso amelazimika kusimamisha ziara yake kwa muda mfupi kusikiliza kero za wananchi wa Kijiji cha Oldonyongiro Wilayani Arumeru kuhusiana na maji ili hali kuna mradi wa maji wa MAKILENGA unaohudumia vijiji 22 kikiwemo kijiji hicho.
Wakitoa malalamiko yao juu ya upatikanaji wa maji Kijijini hapo wananchi hao wamelaani kitendo cha kufungiwa maji na wananchi wenzao wa ukanda wa juu ambapo ndipo mradi unapo anzia ilihali wapo tayari kuchangia gharama za maji.”Kinamama tunateseka tunatumia muda mwingi kufuata maji kwa sababu ya kubaguliwa kwa kufungiwa Maji na watu wa Kata ya Leguruki wanaotumia maji ya bomba kumwagilia”alisema Mwaija Omari.
Mwananchi mwingine alijitambulisha kwa jina la Matayo, amesema uongozi wa bodi ya Maji MAKILENGA umekua ni kikwazo kwani badala ya kutatua changamoto wameendelea kupewa maji kwa mgao ambapo wanaweza kukosa huduma ya maji kwa zaidi ya siku 3.
Aidha Mh. Aweso aliwaomba wananchi hao kuwa wavumilivu na kuendelea na ziara yake inayolenga kutambua na kutatua changamoto za upatikanaji maji kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayo elekeza ifikapo mwaka 2025 upatikanaji maji vijijini kuwa asilimia 85.
Kufuatia malakamiko hayo Naibu huyo ameagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Arumeru kuwashikilia na kuwaweka chini ya ulinzi viongozi wa Bodi hiyo akiwemo mwenyekiti wa Bodi Godhope Chales,Mhasibu wa Mradi Bi.Warialanga Pallangyo,pamoja na fundi bomba anayetambulika kwa jina la Kaaya, kwa tuhuma za ubadhirifu”Serikali haitamfumbia macho yeyote atakaye fanya ubadhirifu wa miradi ya maji na imejikita kuwaletea wananchi maendeleo”amesisitiza Aweso.
Aweso amesema kwa mujibu wa Sheria no 5 ya mwaka 2019 iliyoanzisha mamlaka ya maji vijijini na Mjini RUWASA vyombo vya vya watumia maji ikiwemo MAKILENGA vitaundwa upya hivyo hii itaboresha uongozi pia ameagiza uundaji wa tume itakayochunguza uendeshaji wa mradi huo wa MAKILENGA.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro amesema hakuna tatizo la Maji Kijijini hapo bali tatizo lipo kwa Wananchi wenyewe na uongozi wa MAKILENGA kwani miradi ya maji iliyopo inauwezo wa kuhudumia vijiji vyote 22 vilivyopo kwenye Mradi hivyo ameshauri wenyeviti wa Vijiji vyote 22 kuwa wajumbe wa bodi ili waweze kusimamia upatikanaji wa maji kwenye vijiji vyao.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini Wialaya ya Arumeru mhandisi Christine Kessy amesema kwa mujibu wa Sheria ya Maji no 12 ya mwaka 2009 inaelekeza kuwa, Maji ni rasilimali ya taifa na yanatakiwa yalindwe hivyo hakuna mwananchi anayeruhusiwa kuzuia upatikanaji wa huduma ya Maji pia Sera ya maji ya mwaka 2002 inaelekeza nilazima kwa wananchi wote kuchangia.
Mhandisi Christine ameeleza kuwa Wananchi wa Kata ya Leguruki wamechangia mradi huo kutokufanya vizuri kwani wanatumia maji ya bomba hovyo kumwagilia migomba na kahawa pia hawachangii huduma ya maji.
Ziara ya Mhe.Naibu Waziri wa Maji imekamilika kwa kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, ambapo Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki DKt.John Pallangyo amewashukuru wananchi kwa kumchagua na kuahidi kuwatumikia na kuwawakilisha vyema .
Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki John Pallangyo akizungumza na Wananchi wa Tarafa ya King'ori.
Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki John Pallangyo amewashukuru wananchi hao kwa kumchagua na amehaidi kuwatumikia na kuwawakilisha vyema.pia amewaomba ushirikiano.
ananchi wakimsikiliza Mhe.Mbunge.
Wananchi wakimsikiliza Mhe.Mbunge.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa