Afisa Mipango na Uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Meru Daniel Mwakitalu akiongozana na Afisa maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Meru Frola Msilu wamepata wasaa wakutoa Elimu kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa Mashirika yasiyo yakiserikali Leo Tarehe 27 Septemba 2024 katika Ukumbi wa Semina na mikutano TFFT Uliopo Usa-River.
Aidha Afisa Mipango Amesema kuwa anaamini Mashirika yasiyo yakiserikali Ni miongoni mwa wadau wakubwa watakao weza kupenyeza Elimu Kwa Jamii kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nakuwataka kutumia Nafasi waliyo nayo kufikisha Taarifa hizi za Uchaguzi.
Vivyo hivyo Afisa Maendeleo ya Jamii ameyapongeza Mashirika hayo yaliyoweza kuhudhuria kikao hicho nakusema kuwa Msingi wa Maendeleo katika Jamii zetu ni viongozi hivyo twendeni tukahamasishe Jamii kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili Kupata viongozi Bora watakao kuwa na Tija na watakao weza Kutatua changamoto za Wananchi katika Maeneo yetu.
Kikao hicho cha Mashirika yasiyo yakiserikali kina Lengo la kuangazia changamoto zilizopo kwenye Jamii na kuja na ufumbuzi wa changamoto hizo Kwa kuandaa Mradi mmoja utakaokuwa na uwezo wakutatua changamoto zilizobainiwa kupitia kikao hicho.
Mashirika yaliyo shiriki katika kikao hicho ni Mashirika kutoka Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa