wafanya biashara wa soko la Tengeru Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameunga mkono zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wa mazao barabarani kwa kuwaingiza katika eneo la soko.
Afisa biashara ambaye ni msimamizi wa masoko Elibariki Nnko ameeleza kuwa zoezi hilo limeanza rasmi baada ya baadhi ya wafanya biashara kukaidi kutumia eneo la soko lililojengwa kwa gharama kubwa na kuendelea kupanga bidhaa zao barabarani ikiwa ni kuatarisha maisha yao, pia amefafanua Halmashauri hiyo inaendelea na uboreshaji wa miundombinu kwenye soko hilo kwani mpaka fedha kiasi cha sh. milioni 20 zimetengwa kwa ajili ya kutengeneza meza .
Elisifa Boniface ambaye ni mfanyabiashara kwenye soko hilo amesema wateja wengi hawaingii ndani ya soko kwani hupata mahitaji yao nje ya soko jambo linalo athiri biashara yake na wafanya biashara wenzake waliopo ndani ya soko.
Naye Mary Pallangyo ambaye ni mfanya biashara wa mbogamboga ameiomba Halmashauri hiyo kuboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na kukamilisha uwekaji paa kwenye baadhi ya maeneo.
Na baadhi ya wafanya biashara walio kuwa wakipanga bidhaa zao barabarani wameiomba Serikali kuwaruhusu kuendelea kujitafutia risiki kwa njia hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa