Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Mhe.Jerry Muro wakati wa mkutano na wafanya biashara wa Halmashauri ya Meru,amewahakikishia kuwa Wilaya hiyo itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyabiashara ili waweze kufanya biashara zao bila vikwazo na kulipa kodi kwaajili ya maendeleo ya Taifa .
Mkutano huo ambao umefanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo umekuwaa fursa kwa wafanya biashara hao kueleza changamoto zinazo wasibu kuendesha biashara zao na swala zima la ulipaji kodi ambao wafanya biashara wengi wameomba elimu ya kina juu ya ulipaji kodi kufanyika kabla ya kudaiwa na kuchukuliwa hatua.
Miongoni mwa Changamoto walizotoa wafanya biashara hao ni kutokuwa na uelewa juu ya kodi na tuzo mbalimbali pa wameshauri baadhi ya kodi kuunganishwa ili kuepusha kile walichiita usumbufu.Mmoja wa Wafanya biashara hao Prof.Justine Maeda amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuandaa mkutano huo na kushauri kuwe na muendelezo wa mikutano na wafanya biashara ili waweze kutoa maoni yatakayoiletea mafanikio Wilaya hiyo .
Akihitimisha mkutano huo,Muro amewashukuru wafanya biashara kwa kuitikia wito wa kuhudhuria mkutano huo na kuwasihi kuwa waaminifu kulipa kodi, pia amewaonya watumishi wa Serikali wenye tabia ya kutumia majina ya viongozi kama njia ya kutekeleza majukumu yao kuacha tabia hiyo badala yake watoe elimu ya tozo, Kodi wanazo kusanya kwa kwa wafanyabiashara,"msiwachonganishe viongozi na wananchi"amesisitiza Muro.
Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Hamashauri ya Meru umewakutanisha wafanya biashara wa makundi mbalimbali wakiwemo wamiliki wa viwanda,wamiliki wa maduka,wamiliki wa vituo vya mafuta,wamiliki wa mashamba makubwa,wamiliki wa Hoteli ,wamiliki wa makampuni ya utalii ,wamiliki wa makampuni mbalimbali wamiliki wa vituo /zahanati .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akizungumza na wafanya biashara.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akizungumza na wafanya biashara.
Meneja wa TRA Arumeru akitoa ufafanuzi juu ya ulipaji kodi wakati wa kikao cha Mhe Mkuu wa Wilaya na wafanya biashara.
Baadhi ya Wafanya biashara wakifuatilia mkutano .
Baadhi ya Wafanya biashara wakifuatilia mkutano .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa