Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo amekabidhi tena, fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki kwa Mgina I. Mustafa, wa Chama AAFP. Mgombea huyo alifika kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi majira ya Saa 3:32 asubuhi na kukabidhiwa fomu ya Uteuzi kuwania nafasi ya Mbunge wa Jimbo hilo.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amemkabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.kwenye fomu ya Uteuzi.
Mgombea huyo amefanya kufikisha idadi ya Wagombe watano kutoka vyama vitano vya siasa, kuchukua fomu za Uteuzi wa Ubunge kwa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Ikumbukwe waliochukua fomu za uteuzikugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki ni Shafii M. Kitundu kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (AFDC) , Bi. Gladness M. Kaaya kupitia Chama cha (UPDP) na Ndg. Domina M.Nnko kupitia chama cha Union For Multiparty Democracy (UMD) na Mgina I. Mustafa, wa Chama AAFP.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki Mgina I. Mustafa, wa Chama AAFP.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha AAFP Mgina I. Mustafa, wa Chama baada ya kukabidhiwa fomu ya uteuzi wa kugombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha AAFP Mgina I. Mustafa, wa Chama baada ya kukabidhiwa fomu ya uteuzi wa kugombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa