Wahitimu wa Jeshi la Kujenga Taifa wameaswa juu ya Matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii kwa faida ya Taifa mara baada ya kuhitimu mafunzo ya kujitolea ya operesheni miaka 60 ya jeshi la kujenga Taifa Oljoro.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda ametoa wasaa huo leo alipokuwa akihitimisha mafunzo ya Wahitimu hao.
Kaganda amesema kufuatia ukuwaji wa Maendeleo ya Tekinolojia na utandawazi kila mtanzania anatamani kutumia Simu janja (Smartphone) ambazo zimekuwa na mambo mengi ya mtu kufahamu kile kinachoendelea duniani.
Aidha, ameeleza vijana wengi wamekuwa hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi ya sahihi ya mitandao ya kijamii na kutazama mambo yasiyofaa ambayo ni kinyume na maadili yetu ya Kiafrika.
"Hatukatai kutumia mitandao hiyo ila ni vyema mkatumia mitandao hiyo kwa kujipatia elimu na mambo mema ambayo yatawasaidia katika maisha binafsi na sote kwa ujumla, Serikali yetu imetunga Sheria ya kudhibiti maudhui yasiyofaa mtandaoni ambapo utakapotumia au kuonyesha jambo ambalo ni kinyume na tamaduni zetu hatua kali zitachukuliwa dhidi yako" amesema Kaganda .
Vilevile, Mhe. Kaganda amewapongeza Wakufunzi na viongozi kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwasaidia vijana kutoka kuwa raia wa kawaida hadi kufikia viwango walivyofikia wahitimu wa JKT kwani ni jambo la kujivunia kuwa na jeshi imara na hodari kwa Taifa .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa