Wajasiriamali wadogo Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru wamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John P. Magufuli kwa kutoa vitambulisho maalum kwa ajili yao.
Wakizungumza na mwandishi wetu Wajasiliamali hao wamesema, Vitambulisho hivyo vimekuwa msaada mkubwa kwao katika kufanya biashara zao.
Kwa upande wa Thadeo fundi viatu kutoka Kata Usa - River amemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa vitambulisho hivyo vinavyowarahisishia kufanya biashra zao bila kupata usumbufu wowote "tunajivunia kufanya biashara tukiwa tunatambulika ni heshima na tupo salama kufanya biashara sehemu yoyote "amesema Thadeo.
Aidha Thadeo ametoa wito kwa Wajasiliamali wadogo wanaokwepa kuchukua vitambulisho hivyo kuacha tabia hiyo ili waweze kufanya biashara bila usumbufu.
Naye Vumilia shoo muuza matunda maeneo ya Leganga amesema vitambulisho hivyo vimekua fursa tosha kwa wanawake kujikwamua kiuchumi kwa kufanya biashara bila usumbufu wowote .
Vumilia amesema kwa sasa wanapata faida kubwa tofauti na awali ambapo walikuwa wakifukuzwa wanapopanga bidhaa zao maeneo mbalimbali hivyo kupoteza muda mwingi kujificha badala ya kufanya biashara.
Sambamba na hilo wajasiriamali hao wameiomba Halmashauri kupitia Idara husika kuendelea kutoa elimu ya Biashara kwa wajasiriamali wadogo ili waweze kukuza mitaji yao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Emmanuel Mkongo amewaasa watendaji wa Kata na Vijiji kutotumia fedha za Vitambulisho vya wajasilimali wadogo kwenye matumizi yoyote bali kuwasilisha fedha hizo ofisi husika.
Pia Mkongo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Meru imerahisisha zoezi la utoaji Vitambulisho vya wajasiliamali wadogo kwa kuwapelekea maeneo yao ya biashara.
Ikumbukwe kuwa, Tarehe10 Disemba 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt John Pombe Magufuli alitoa vitambulisho maalum kwa ajili ya Wajasiliamali wadogo na kuelekeza kuchangia gharama za utengenezaji wa vitambulisho hivyo kiasi cha tsh 20,000 tu ambapo watafanya biashara zao kwa uhuru kwa mwaka mzima.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa