Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo amekabidhi tena, fomu za Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki wateule watatu, Shafii M. Kitundu kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (AFDC) , Bi. Gladness M. Kaaya kupitia Chama cha (UPDP) na Ndg. Domina M.Nnko kupitia chama cha Union For Multiparty Democracy (UMD).
Wagombea wote watatu wa walifika kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi kwa nyakati tofauti na kukabidhiwa fomu hizo za Uteuzi kuwania nafasi ya Mbunge wa Jimbo hilo.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, alimkabidhi fomu za uteuzi wa nafasi ya Ubunge Shafii M. Kitundu kupitia Chama cha (ADC) mnamo saa 9:35 asubuhi. Pia Bi. Gladness M. Kaaya Chama (UPDP) alikabidhiwa fomu hizo majira ya saa 6:46 mchana na Domina M.Nnko wa chama cha UMD alikabidhiwa fomu hizo majira ya saa 8:41 mchana.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amewakabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.kwenye fomu ya Uteuzi.
Wagombea hao watatu wamefanya kufikisha idadi ya Wagombe wanne kutoka vyama vitatu vya siasa, kuchukua fomu za Uteuzi wa Ubunge kwa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki Shafii M. Kitundu kupitia Chama cha ( ADC).
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki Domina M.Nnko kupitia chama cha Union For Multiparty Democracy (UMD).
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo akimkabidhi fomu za Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki Bi. Gladness M. Kaaya Chama (UPDP)
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa